Arusha: Askari SUMA JKT wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Arusha: Askari SUMA JKT wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Pununkila

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2021
Posts
689
Reaction score
1,706
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia askari watatu wa Suma JKT kwa tuhuma za kumtesa hadi kumuua mkazi wa eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Almasi Mohamed wakimtuhumu kwa wizi wa mahindi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Jastine Maseju akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Septemba 7, 2021 amesema watuhumiwa hao ni walinzi shamba la Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mbegu za Kilimo (ASA) lililopo eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru.

"Ni kweli tunawashikilia askari watatu wa Suma JKT na upelelezi unaendelea wa tukio hili la mauaji na tutatoa taarifa rasmi baada uchunguzi kukamilika,"amesema.

Mke wa marehemu, Mwanahamisi Rajabu amesema mume wake kabla ya kufariki juzi alikuwa na majeraha ya kipigo na alilazwa katika hospitali ya Olturumet akiwa anatapika damu.

"Nilipigiwa simu na polisi kuwa mume wangu amelazwa hospitali anaumwa sana kutokana na kipigo nikaenda na kumkuta ana hali mbaya na akanieleza kwa taabu kilichotokea na baadaye akafariki,"amesema.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Seuli, Elias Ndemlya amesema marehemu alikuwa ni mkazi wa eneo lake akijihusisha na kilimo na aliwahi kuwa mfanyakazi katika shamba hilo

"Hili sio tukio la kwanza baadhi ya askari wa Suma JKT wanaolinda shamba kupiga watu na kujeruhi wakiwatuhumu ni wezi tunaomba Serikali ichukuwe hatua kukomesha ukatili huu,"amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hao jamaa ni ushamba na zile sifa za kijinga kwamba wao ni kiboko ndio vinawaponzaga, kiukweli mtu uliyehitimu mafunzo ya kijeshi (jkt,jwtz, polisi, magereza nk) huwezi kujifanya wewe ni mweredi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwa kibaka asiye na mafunzo yoyote na tena asiye na silaha yoyote ukaamua kumtesa kama unapambana na mwanajeshi mwanzako adui mliokutana uwanja wa vita.
 
Hao jamaa ni ushamba na zile sifa za kijinga kwamba wao ni kiboko ndio vinawaponzaga, kiukweli mtu uliyehitimu mafunzo ya kijeshi (jkt,jwtz, polisi, magereza nk) huwezi kujifanya wewe ni mweredi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwa kibaka asiye na mafunzo yoyote na tena asiye silaha yoyote ukaamua kumtesa kama unapambana na mwanajeshi mwanzako adui mliokutana uwanja wa vita.
Askari wetu wapewe hata vita ya kirafiki na nchi nyingine wazichape wamalize hamu zao maana wanakuwa na uonevu mwingi kwa raia.
 
Hizo ni stress za kutoka JKT na kukosa chance za kujiunga na JW, Polisi,uhamiaji,Tiss wamejikuta wameangukia kwny ulinzi.
 
Walinzi wa SUMA JKT ni matatizo, wana stress nyingi hadi kufikia hatua kujiona wana maamuzi ya kujichukulia sheria mkononi. Tatizo mfumo uliwabeba sana sasa unawatema
 
Niliwahi kuandika uzi kuhusu hawa walnzi wa suma jkt.
Kwa ufupi hawa vijana ni matokeo ya mfumo wa kinyonyaji wa serikali ya Tanzania.
 
Infiriority complex inawatafuna vijana wa Suma Guard..

Wanajua Askari wa kampuni binafsi wanaonekana si kitu kwa jamii na wao kwa bahati mbaya wameingia huko baada ya kukosa nafasi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama hivyo inawabidi walazimishe heshima..

Si ajabu kumkuta kijana wa Suma Guard akigombana na konda wa daladala kuwa yeye ni Askari hivyo asilipe nauli..
 
Hawa SUMA JKT huwa wanajiona kama Makomando wa Guinea sana hawa.
 
Ahooo jamaa wana2mia nguvu sehemu ambayo haitajikii ku2mia nguvu.... Kuna tawi flan la benk niliendaa wakaanza kunileteaa fyok fyok na kunitishia kunipiga... Niliwapa jibu Moja tu... Mpaka leoo wakiona wanaishia kuniangalia2....
 
Ahooo jamaa wana2mia nguvu sehemu ambayo haitajikii ku2mia nguvu.... Kuna tawi flan la benk niliendaa wakaanza kunileteaa fyok fyok na kunitishia kunipiga... Niliwapa jibu Moja tu... Mpaka leoo wakiona wanaishia kuniangalia2....
Dah una bahati kweli,
Wala usijaribu tena kujibizana nao
 
Back
Top Bottom