Arusha: Auwawa kwa kupigwa na kitu kizito baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Jamani wanaJukwaa. Huku kuingilia mapenzi ya watu na kujifanya mwema wakati mwingine tuangalie na kuwa makini
==============
Mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la Akwii ambaye ni mlinzi na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kilichodhaniwa kuwa nondo mara baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake akitaka kusuluhisha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba Akwii alikwenda kusuluhisha ugomvi uliokuwa wa mda mrefu kati ya wapenzi hao kitendo ambacho kijana mwenye mchumba hakufurahishwa na kitendo hicho na baadae kurudi na kuamua kumpiga na nondo na hatimae kupelekea umauti wake.

Soma Pia:
“Huyu ni mzee mlinzi wa kijiji hapa ameuwawa aliingilia ugomvi wa mdada ambae alikuwa akigombana na mme wake. Yeye alikwenda kumfata mlinzi mwenzake usiku na wakati wanarudi lindoni kwake wakakuta ugomvi usiku ndo akamwambia mwanaume acha kugombana na huyo dada huku akimtetea na ndipo mwanaume akamuweka alama akaja baadae akamvizia na kumpiga na nondo akafariki” Amesema David mkazi wa Kimandolu

Wakazi wa kimandolu wameeleza kuguswa na kifo cha mlinzi huyo na tayari tukio hilo limesharipotiwa kituo cha polisi kwa ajili ya uchunguzi Zaidi.
 
Marehemu apumzike kwa amani. Marehemu alikua mtu mwenye roho nzuri na mpenda amani, hakutaka kuona mwanamke anapigwa, akataka amani, akasuluhisha.

Huyo kenge akaamua kumvizia marehemu na kumuua, mtu wa hovyo sana. Kama alikua mwanaume kweli alitakiwa azipige pale pale na marehemu badala ya kumvizia off guard na kumuua. Hovyo sana.
 
Arusha sio tu kuingilia ugomvi ndio Mji una watu wagomvi nadhani kupita maeneo mengi niliyowahi kuishi na vituo vya Hiace wahuni wanatukana matusi makubwa kuliko maelezo na hawajali kabisa hayo matusi wangetukana Mkoa wa Mbeya wangekula bakora za kutosha ila huko wao ndio wana nguvu na raia wanaangalia tu huku wakitukana mbele ya wapita njia Arusha bado wana ule ubabe wa kizamani sana na hawataki kushindwa hata kwa ugomvi wa kijinga.
 
Siyo Akwii bali ni Akui. Kumaanisha mjomba kwa lugha ya Kimasai. Hivyo, hapo jina la mhusika halipo.

Kesi hii mhusika akaombe kumaliza kimila.

Utaratibu ni kuwa, mhusika atazikwa na kikao kukaa. Kisha muuaji ataitwa pamoja na ukoo wake.

Ili kumaliza utata, atapaswa kulipa ng'ombe 49.

Na hizo ng'ombe haziletwi mchana wala asubuhi, bali ni usiku wakati pengine sehemu kubwa ya watu wamelala.

Na ng'ombe hizo hazilipwi mpak pale ambao aliyefariki ataaminika ameshaoza na wadudu washafaidi chai. Pengine ambacho kimebakia ni mifupa tu.

Njia hii hutumika kama kusafisha muuaji na kizazi chake. Isipofanyika hivyo, familia ya muuaji itaendelea kuteketea mpaka kizazi cha nne. Ila ikifanyika basi laana ya kuondoa uhai wa mtu unaishilia kwa muuaji pekee.

Ni dhambi Moja kuu katika kabila la Wamasai.

Alamsiki.
 
Kwahiyo serikali itafumbia macho mkuu?
 
Kuna siku narudi maskani mdogomdogo pembezoni mwa barabara jamaa kasimama na demu wake anacomplain jinsi demu anavyomdharau pamoja na kumhudumia. Ile nawafikia kwa ukaribu zaidi namsikia demu anajibu kwa vihela gani unavyonipa.

Hapo vikaanza kutembezwa vitasa huku mimi sauti inaniambia, "Private, do not engage, i repeat do not engage.". Nikawapita kama kuhani mkuu.

Walikuja kuachanishwa na bodaboda.
 
Jamani wanaJukwaa. Huku kuingilia mapenzi ya watu na kujifanya mwema wakati mwingine tuangalie na kuwa makini
==============
Mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la Akwii ambaye ni mlinzi na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kilichodhaniwa kuwa nondo mara baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake akitaka kusuluhisha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba Akwii alikwenda kusuluhisha ugomvi uliokuwa wa mda mrefu kati ya wapenzi hao kitendo ambacho kijana mwenye mchumba hakufurahishwa na kitendo hicho na baadae kurudi na kuamua kumpiga na nondo na hatimae kupelekea umauti wake.

Soma Pia:
“Huyu ni mzee mlinzi wa kijiji hapa ameuwawa aliingilia ugomvi wa mdada ambae alikuwa akigombana na mme wake. Yeye alikwenda kumfata mlinzi mwenzake usiku na wakati wanarudi lindoni kwake wakakuta ugomvi usiku ndo akamwambia mwanaume acha kugombana na huyo dada huku akimtetea na ndipo mwanaume akamuweka alama akaja baadae akamvizia na kumpiga na nondo akafariki” Amesema David mkazi wa Kimandolu

Wakazi wa kimandolu wameeleza kuguswa na kifo cha mlinzi huyo na tayari tukio hilo limesharipotiwa kituo cha polisi kwa ajili ya uchunguzi Zaidi.
Sasa huyo jamaa alieua, atakosa mchumba maana ataozea jela. Sasa ujinga Gani huo? Halafu mambo ya kuwa wapenzi kabla ya ndoa sisi waislam tumekatazwakabisa, athariyake ndio hii
 
Back
Top Bottom