Arusha: Auwawa kwa kupigwa na kitu kizito baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake

Arusha: Auwawa kwa kupigwa na kitu kizito baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake

Siku hizi hata nikikorofishana na mtu huwa naondoka naenda zangu mbalii, mambo ya kuingilia ugomvi ndio sijawahi mtu mwenyewe muoga. Watu wengi ni wagonjwa wa akili kuuliwa siku hizi ni kama kunywa maji.
 
Tatizo Arusha wahuni Ni wengi,watu wengi Arusha wanaona prestige kuwa muhuni.
 
Siyo Akwii bali ni Akui. Kumaanisha mjomba kwa lugha ya Kimasai. Hivyo, hapo jina la mhusika halipo.

Kesi hii mhusika akaombe kumaliza kimila.

Utaratibu ni kuwa, mhusika atazikwa na kikao kukaa. Kisha muuaji ataitwa pamoja na ukoo wake.

Ili kumaliza utata, atapaswa kulipa ng'ombe 49.

Na hizo ng'ombe haziletwi mchana wala asubuhi, bali ni usiku wakati pengine sehemu kubwa ya watu wamelala.

Na ng'ombe hizo hazilipwi mpak pale ambao aliyefariki ataaminika ameshaoza na wadudu washafaidi chai. Pengine ambacho kimebakia ni mifupa tu.

Njia hii hutumika kama kusafisha muuaji na kizazi chake. Isipofanyika hivyo, familia ya muuaji itaendelea kuteketea mpaka kizazi cha nne. Ila ikifanyika basi laana ya kuondoa uhai wa mtu unaishilia kwa muuaji pekee.

Ni dhambi Moja kuu katika kabila la Wamasai.

Alamsiki.
Vp kama police wataingilia na mtuhumiwa kufungwa. Je family yake itaendelea na huo utalatibu WA kulipa ng'ombe
 
Back
Top Bottom