Siyo Akwii bali ni Akui. Kumaanisha mjomba kwa lugha ya Kimasai. Hivyo, hapo jina la mhusika halipo.
Kesi hii mhusika akaombe kumaliza kimila.
Utaratibu ni kuwa, mhusika atazikwa na kikao kukaa. Kisha muuaji ataitwa pamoja na ukoo wake.
Ili kumaliza utata, atapaswa kulipa ng'ombe 49.
Na hizo ng'ombe haziletwi mchana wala asubuhi, bali ni usiku wakati pengine sehemu kubwa ya watu wamelala.
Na ng'ombe hizo hazilipwi mpak pale ambao aliyefariki ataaminika ameshaoza na wadudu washafaidi chai. Pengine ambacho kimebakia ni mifupa tu.
Njia hii hutumika kama kusafisha muuaji na kizazi chake. Isipofanyika hivyo, familia ya muuaji itaendelea kuteketea mpaka kizazi cha nne. Ila ikifanyika basi laana ya kuondoa uhai wa mtu unaishilia kwa muuaji pekee.
Ni dhambi Moja kuu katika kabila la Wamasai.
Alamsiki.