Cyurinyana
Member
- Aug 30, 2026
- 38
- 36
Binti anayefahamika kwa jina la Irene, mwenye umri wa miaka (24), mkazi wa Mtaa wa Lemara, Kata ya Lemara, Jijini Arusha, amefariki dunia baada ya kudaiwa kujeruhiwa kwa chupa wakati akiwa pamoja na wenzake katika eneo la The HUB.
Mama mzazi wa Irene, Mariam Selemani, amesema marafiki wawili wa binti yake walifika nyumbani leo Septemba (14), saa (12) asubuhi, na kumjulisha kuwa Irene alikuwa amejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini, ambako alifariki. Mariam amesema alipofuatilia tukio hilo alipewa maelezo yanayotofautiana, kwani awali aliambiwa kulikuwa na ugomvi, huku baadaye akielezwa kuwa wenzake hawakumuona Irene walipotoka hadi walipomkuta amelala nje huku damu ikimtoka.
Rehema Ramadhan, aliyemlea Irene tangu akiwa mdogo, amesema marehemu alikuwa mtoto mzuri na asiye na matatizo, huku akieleza kuwa taarifa ya kifo chake imepokelewa kwa maumivu makubwa.
Baada ya kufika The HUB, wafanyakazi walieleza kuwa meneja alikuwa kituo cha polisi. Akizungumza kwa simu, Meneja Paulo amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa kumi, lakini lilitokea nje ya geti la klabu hiyo.
Soma Pia: Arusha: Binti adai kuvuliwa nguo na kuchomwa na pasi na mwajiri wake
Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha Irene, huku ikiwekwa wazi kuwa watu wawili waliokuwa pamoja naye wanashikiliwa kwa mahojiano ili kusaidia kubaini mazingira ya tukio hilo.