Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Vijana wanaojiita Arusha boys ambao wameweka kambi eneo la wazi la makaburi karibu kabisa na stand kubwa ya mabasi ya mikoani wamekuwa wakiuza Gongo mchana kweupe kwa staili ya aina yake,
Gongo hiyo huwekwa kwenye chupa maalumu za maji ya kunywa na pindi mteja anapokuja kutaka huduma hupimiwa kwenye bilauri na hunywa kwa kujiachia kama mtu anaekunywa maji.
Wateja wao wakubwa ni wapiga Debe, Machinga, wachora kucha,waokota chupa Na baadhi ya wapita njia.
Vijana hao huanza kazi yao asubuhi na mapema hadi muda wa saa moja usiku.
Staili yao ya biashara ni ngumu kwa mpita njia kujua kama kuna biashara inayoendelea hapo kutokana na mazingira, kwanza kabisa pametandikwa karatasi safi pamoja na viroba vichafu ambavyo hutumika kuficha chupa hizo zenye kinywaji pamoja na bilauri, na hutolewa tu pale mteja anapohitaji huduma
mteja akiwa anapatiwa huduma hiyo
biashara ikiendelea