Arusha: Eneo la wazi la makaburi Gongo inapouzwa na kunywewa wazi wazi

Arusha: Eneo la wazi la makaburi Gongo inapouzwa na kunywewa wazi wazi

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Vijana wanaojiita Arusha boys ambao wameweka kambi eneo la wazi la makaburi karibu kabisa na stand kubwa ya mabasi ya mikoani wamekuwa wakiuza Gongo mchana kweupe kwa staili ya aina yake,

Gongo hiyo huwekwa kwenye chupa maalumu za maji ya kunywa na pindi mteja anapokuja kutaka huduma hupimiwa kwenye bilauri na hunywa kwa kujiachia kama mtu anaekunywa maji.
Wateja wao wakubwa ni wapiga Debe, Machinga, wachora kucha,waokota chupa Na baadhi ya wapita njia.

Vijana hao huanza kazi yao asubuhi na mapema hadi muda wa saa moja usiku.

Staili yao ya biashara ni ngumu kwa mpita njia kujua kama kuna biashara inayoendelea hapo kutokana na mazingira, kwanza kabisa pametandikwa karatasi safi pamoja na viroba vichafu ambavyo hutumika kuficha chupa hizo zenye kinywaji pamoja na bilauri, na hutolewa tu pale mteja anapohitaji huduma
DSC_0881.JPG
mteja akiwa anapatiwa huduma hiyo
DSC_0868.JPG
biashara ikiendelea
 
Ingawa haileti picha nzuri katikati ya jiji na ni vema wakaondolewa hii ni pamoja na msongamano wa machinga uliojaa mitaa hio, Anyway waache masikini wapate faraja yao na hii ni kutokana na matabaka tuliyojiwekea wenyewe
 
Kwa vyovyote Wateja ni wanaojuana vizuri ndio maana hawana shida na kuonesha bidhaa yao kwa Wateja wapya.
 
Hata pale chini maeneo ya Jogoo House kulikuwa kuna kijiwe cha mbege, ila nadhani nao wamekuwa Wahanga wa hili zoezi la 'ondoa Machinga mjini'.
 
Hata pale chini maeneo ya Jogoo House kulikuwa kuna kijiwe cha mbege, ila nadhani nao wamekuwa Wahanga wa hili zoezi la 'ondoa Machinga mjini'.
Ile mbege ya pale ilikuwa inatokea kibosho, saa kumi na moja alfajiri mbege ishafika Arusha
 
Ile mbege ya pale ilikuwa inatokea kibosho, saa kumi na moja alfajiri mbege ishafika Arusha
Na Waarabu wa Pemba walikuwa wanajuana kwa vilemba vyao.

Ukikaribia maeneo unasikia harufu ya mbege na maongezi "laalu le mbe....." unajua kabisa hapa hapanihusu unachapa lapa.
 
Nimemiss harufu ya gongo kinoma[emoji39][emoji39][emoji39]

Hii kitu ina addiction zaidi ya cocaine....

Nimeinywa miaka kama 10 iliyopita lkn mpaka sasa harufu yake haijanitoka kichwani.
 
Nimemiss harufu ya gongo kinoma[emoji39][emoji39][emoji39]

Hii kitu ina addiction zaidi ya cocaine....

Nimeinywa miaka kama 10 iliyopita lkn mpaka sasa harufu yake haijanitoka kichwani.
Hao vijana wanoukunywa hapo ukiwacheki vizuri wamechoka sana miili yao na ngozi yao pia imekosa nuru kabisa
 
Usiseme gongo sema supu ya maninja alaf wangekua wanauza wine hadharan wala hata msinge wachoma ila kwakua wanakula kitu Cha asili maneno ndo inakua mingi
 
Back
Top Bottom