Nabii wa Mungu, Godbless Lema, leo amekitendea haki Cheo Chake cha Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, baada kuwatimulia mbali Maofisa wa TAKUKURU waliohudhuria semina ya Wagombea wa Uenyekiti wa Serikali za Mitaa.
Nabii Lema ambaye Unabii wake juu ya Mambo kadhaa ya Tanzania Umetimia na kupitiliza, amewaambia Maofisa hao wa TAKUKURU kwamba Wameacha uozo kwenye Uandikishaji uliofanywa na viongozi wa serikali halafu wanakimbilia kuleta pua zao kwenye Semina zisizo na Makando kando za Chadema.
View attachment 3146379View attachment 3146382View attachment 3146387
Binafsi Naunga Mkono Jambo hili
=====
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amewafukuza maofisa watatu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwenye semina ya wagombea wa wenyeviti wa mitaa wa chama hicho.
Lema aliyekuwa mgeni rasmi leo Novemba 7, 2024 katika mkutano huo jijini Arusha, baada ya kuingia ukumbini na kupata utambulisho kuhusu uwepo wa maofisa wa Takukuru waliokuwa meza kuu, alisimama na kusema hakubaliani na uwepo wao.
"Sitakubali muongee na wajumbe wetu wakati mmeshindwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wa serikali wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao pia waandikishaji wa daftari la wapiga kura kwa vitendo walivyokuwa wanafanya hivyo naombeni muondoke hatuwahitaji hapa,”alisema Lema.
Hata hivyo maofisa hao waliokuwa wamekaa meza za mbele kwa wageni rasmi hawakunyanyuka hadi wasimamizi wa ulinzi wa semina hiyo walivyowafuata na kuwanyanyua kwa nguvu ndipo wakaamua kutoka huku wakizomewa na ukumbi mzima.
Akizungumzia hali hiyo, kwa njia ya simu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo amesema suala hilo si jema lakini haliwezi kuzuia elimu ya rushwa kuwafikia wananchi.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi