Arusha: Jeshi la Uokoji (Zimamoto) lashindwa kumuokooa kijana kisimani hatimaye kufariki

Arusha: Jeshi la Uokoji (Zimamoto) lashindwa kumuokooa kijana kisimani hatimaye kufariki

Askari pesa
Jeshi la Uokoaji (Zimamoto) Mkoani Arusha, limeshindwa kumuokoa kijana aliyeshindwa kutoka kisimani hali iliyopelekea afie ndani ya kisima hicho.

Baada ya Jeshi la Uokozi kushindwa kumtoa kijana huyo, ndipo akatafutwa kijana amabye alilipwa kiasi cha Shilingi Laki Tatu na kufanikiwa kutoa mwili wa marehemu.

Kijana huyo aliingia katika kisima hicho chenye urefu wa mita 60 ili kumtoa mbuzi aliyekuwa ametumbukia akiahidiwa kulipwa kiasi cha shilingi elfu 40.

Pia soma Arusha: Afariki baada ya kuingia kwenye kisima chenye mita 60 kumtoa mbuzi

View attachment 3208830

Chanzo: Ayo Tv.
Askari pesa wakiwa na vifaa wameshindwa kumuokoa kijana raia asiyekua hata na mtungi wa O² kufanikisha zoezi Dah aise haya ni maajabu
 
Habari ni ya kweli, nimecheki ayo tv
Ndio ila alikufa siku Ile Ile na ilikuwa usiku...sio kwamba zimamoto wamesababisha afe..zimamoto walitaitwa waje kutoa mwili tu sio kutoa mtu aliye hai
 
Kijana huyo aliingia katika kisima hicho chenye urefu wa mita 60 ili kumtoa mbuzi aliyekuwa ametumbukia akiahidiwa kulipwa kiasi cha shilingi elfu 40.
Duuuh hicho kisima kama ni mita 60 kwenda chini straight, hicho ni hatari sana otherwise ni 60Fts
 
Nimeelewa mkuu ndo nikaona kuna maajabu fulani hivi pesa juu ya pesa. Huyu wa laki tatu nae asingetoka dau lingepanda pia. Ni kufa kufaana
Angetokea mwingine kudai dau la milioni moja kumtoa marehemu binadamu na marehemu mbuzi. Hatari sana
 
Sasa hilo jeshi la uokozi lina faida gani kama kijana mmoja ambaye hana mafunzo ameweza kutekeleza kazi iliyowashinda askari walioko eneo la tukio?
Siku ya tukio nililisema hili,watu wakaanza kusema mita 60 ni parefu sana

Lakin kijana asie na mafunzo ya uokozi kaweza hyo kazi

Hii nchi hakuna atakaechukuliwa hatua hapo na maisha yataendelea kama kawaida,walijitahid kufika kwa wakati lakin vitendo sifuri
 
watoto wa 2000 hawawezi kuelewa hii lugha..maana ufundi huu wa lugha tuliufaidi kwenye vitabu vya marehemu Shaaban Robert alikuwa fundi wa kiswahili huyu mzee vitabu vyake havichoshi kusoma
Hakika, ndugu.
 
Sasa hilo jeshi la uokozi lina faida gani kama kijana mmoja ambaye hana mafunzo ameweza kutekeleza kazi iliyowashinda askari walioko eneo la tukio?
Nae wamchukue tu ajiunge nao kama Majaliwa mzee wa Kasia.

Inaonesha mafunzo wanayopewa hao askari zimamoto hayatoshelezi.
 
Back
Top Bottom