Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
kila panapokucha panakucha na toleo jipya la pombe ,
Kuna ongezeko la kutisha la viwanda bubu majumbani vya utengenezaji wa kila aina ya pombe za makopo ambazo hazina viwango,jambo ambalo linahatarisha usalama wa wananchi hususani vijana.
Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika serikali kushindwa kudhibiti ongezeko kubwa la viwanda bubu vya pombe za makopo ambazo hazina viwango wala ubora na kuhatarisha afya za vijana walio wengi na kupoteza nguvu kazi kubwa.
Baadhi ya watu wamekuwa wakitengeneza pombe hizo majumbani kwao na kusambaza katika maduka
ya mtaani pamoja na bar ama vilabuni.
Pombe hizo za makopo hazina viwango maalumu cha kilevi wala ubora na wanywaji wengi huishia kuvimba mashavu pamoja na kushindwa kufanya kazi ngumu.