KERO Arusha: Kuna uchafuzi mkubwa wa mazingira unafanyika maeneo ya Friends Conner na Soko la Samunge

KERO Arusha: Kuna uchafuzi mkubwa wa mazingira unafanyika maeneo ya Friends Conner na Soko la Samunge

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
IMG_20240524_083414_392.jpg
IMG_20240524_083124_637.jpg
Habari, wanaouza viungo vya chakula, mboga za majani, matunda na bidhaa nyinginezo maeneo ya barabarani hasa maeneo ya friends Conner Arusha na maeneo ya soko la Samunge upande wa chini mwa soko mbele ya kituo cha kurekebisha tabia za watoto(magereza ya watoto Arusha) wapo watu wanaofanyia biashara eneo Hilo wamekuwa wakichafua mazingira Kwa KIASI kikubwa wanaacha hapo mabaki ya bidhaa zao nyakati za jioni wanamwaga maji hovyo hivyo mazingira yanabakia machafu.

Wapo wanaoshea matunda, mihogo na viazi kwenye mitaro ya maji taka pasipo kujali afya za walaji, pia wapo wanaojisaidia pembezoni mwa eneo Hilo jambo ambao ni hatarishi Kwa afya za wananchi.

Pia wamekuwa kero Kwa watumiaji wa Barbara eneo la barabara limekuwa finyu kutokana na wao kufanyia biashara barabarani wanaweza pia kusababisha ajali, pia wanapanga bidhaa zao mbele ya wenye maduka ambao ni walipakodi HALALI...

Ninaomba mamlaka HUSIKA kufanyia kazi hili ikiwezekana wahamishiwe sehemu zingine na wafuate kanuni za utunzaji wa mazingira na wanapouza bidhaa hasa vyakula wasiweke chini barabarani kwani Kuna majitaka yanachafua vyakula hivyo vilevile vile wasitupe taka hovyo.
 
Back
Top Bottom