ARUSHA KWA YESU: Hatimaye jiji limeangukia mikononi mwa mitume na manabii

ARUSHA KWA YESU: Hatimaye jiji limeangukia mikononi mwa mitume na manabii

temoin

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2025
Posts
311
Reaction score
708
Geneva of africa is fall down

Lile jiji lililofahamika kama ngome ya upinzani na kitovu cha utalii africa sasa limekuwa pango la matapeli kwa wanaojiita manabii na mitume uchwara wanaotumia kivuli cha dini kufanya utapeli.

Wanauzia watu maji na mafuta wanayowaaminisha watu kuwa ni ya upako na kuna wengine wanauzia watu udongo wakiwadanganya kuwa ni udongo wa israeli eti ukiuchanganya na udongo wa sehemu unapokaa ardhi yako itabarikiwa., huwa najiuliza ni lini huyo mtu alienda israeli kuchukua huo udongo na ni wapi amepata kibali cha kufanya biashara kwa kutumia udongo wa nchi nyingine, huu ni wizi na ni utapeli wa waziwazi unaofanywa na baadhi ya watu kupitia dini.

Arusha kuna sehemu kuu nne ambazo watu wanapigwa hela kwelikweli na kila mmoja ameteka eneo lake kwa ajili ya hzo huduma zao wanaoziita za kiroho.
KISONGO kwa geo devi, MBAUDA safina, KALOLENI shalom na NJIRO kwa onesmo . Hao ni majayanti wanne ambao wameliteka jiji la arusha achilia mbali hawa wengine wadogo wadogo wanaotembea barabarani kutwa nzima kutafuta riski kwa kujifanya wanahubiri injili.

Ifike wakati serikali iangalie hili swala kwa jicho la tatu maana kinachoendelea kwenye hayo makanisa ni zaidi ya utapeli, inafikia hadi kipindi wananunuliwa hadi watu wa kutoa ushuhuda ili tu kumpa umaarufu nabii fulani ili apate wafuasi wengi na kuna mmoja kanisa lake lina hadi sehemu ya VVIP.

Wanachofanya hawa jamaa siyo dini bali ni biashara na utapeli
 
Usichokijua, serikali ndio waasisi na walezi.
Watu wapumbazwe wawe wapumbavu.
 
kikubwa ni maamuzi ya mtu binafsi kama rais wako alienda kwa mwamposa ww unaumia nini?
~hakuna jiji lenye kizazi cha hovyo kama arusha wanahitaji zaidi ya maombi ili kuleta reform.
 
Back
Top Bottom