Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Watz watu wa ajabu sana,hapo wengi kama mnafurahia hivi Sabaya kugeuziwa kibao.
Mi sioni hata baya alilofanya.
Mengi kafanya kutimiza majukumu yake, hayo ya pombe na malaya kwa umri wake ataacha vipi na hela na madaraka anayo?
Hapo ni fitnafitna tu tusishangilie upuuzi, mi nishawekwa ndani sana tu kwa kesi kutishia kuua za kubumba,nikahama nchi miaka 10 narudi maafisa uhamiaji wakaomba hongo Airport 2 hapo nikawanyima nikabambikiwa kesi ya madawa.
So hayo mambo kibongo yanaweza kumkuta yoyote saa yoyote, msikitikie mwenzio unapoona anapelekwa kule sio kufurahi,
Yanaweza kukukuta saa yoyote hapo,
Kuna siku pia naenda kwa mama hapo buguruni kituoni cha basi hao polis kmmk wametoka kushika vibaka huko wakaniunganisha nao nawaeleza nimetoka kazini nasubiri basi aah wapi hawaelewi ,
Nikawekwa lokapu baada kusachiwa wakakuta nna hela kibao na simu samsung slide miaka hiyo.
Wakalamba elfu 80(nyingi miaka hiyo),
na simu hawakurudisha.
Nikaambiwa tu njoo vaa viatu kimbia, yaani niliporwa na polisi.
Basi kuepusha shari nikatimka.
So uonevu, kubambikiwa kupo sana huko usifurahie mwenzio yanapomkuta anytime inaweza kukukumba.
 
Mkuu Tanzania ina wilaya ngapi Hadi iwe kwa Sabaya tu? Ma dc wengine walikuwa hawafanyi kazi?
Je, kutishia kuua Watanzania wenzetu ndo kazi za dc?,Je kujihusisha na vitendo vya rushwa,matumizi mabaya ya ofisi ya umma, kutumia bunduki za Watanzania kufanya ujambazi na unyang'anyi wa Mali za Watanzania wenzetu?Haya ndo majukumu ya dc?
Pia mkuu acha kujiondoa ufahamu,ujambazi na ukatili wa huyu jamaa ulitapakaa kila kona hata wanaochunguza habari za huyu jambazi walikuwa nazo siku nyingi.
 
Sijui hata kama umesoma ulichokiandika hapa? Yaani issue ya Sabaya anaonewa na polisi au mamlaka iliyomuweka hapo Hai? Mlishupaza shingo wakat watu wanalalamikia uonevu wa Sabaya na kibaya zaid mkahisi kina Sabaya wana haki ya kuishi kuliko wengine.
Kutokana na story yako hapa wewe ni above 40, sasa kwa umri huo mlitakiwa kumkemea Sabaya kipindi anaiongoza Hai lakni kwa ujinga wenu mlimuangalia Mbowe kama target mkasahau kuwa Sabaya anachupa mipaka anahitaji kukemewa afate sheria.
CCM ya Magufuli iliwafundisha vijana tabia chafu sana kwa kisingizio cha uzalendo, mliwatuma vijana wachape watu hadharan, watishie kutoa roho za watu wanaotoa maoni kinyume, walitukana hadharani na kulindwa na polisi, maovu yote hayo mliyafanya sheria bila kujali maumivu ya wengine.
Muombeeni Sabaya msamaha tu kama binadamu ila sheria ifate mkondo wake.
 
Unaongea nini?Huyo Sabaya atashughulikiwa kwa makosa yake,i dont care.
Mbowe na Sabaya hawapishani chochote.
Ashafanya sana ufirauni pale bills kwa mabinti mabarmaid.
Anyway mi si mwanasiasa wala sishabikii chama chochote.
Sabaya akikutwa na mashtaka ashitakiwe,
ila sijapenda watu kushadadia hilo
Inaweza kukukuta hata wewe saa yoyote.
 
Hii ni picha ya utawala wa mwendazake ,
 
Kwahio ni ka-utaratibu fulani Je kautaratibu hako ni kazuri..., au ni kushushiana hadhi kwa mtuhumiwa kufanywa kama mharifu ? Samahani hata ilivyotokea kwa kina Rugemalila na yule kibaka wa kuku na simu sikusema ila sio kwamba nilifurahishwa..., Hii yote ni kujitayarisha na sisi potential watuhumiwa (mimi, wewe na yule) siku yakitukuta tupelekane kistaarabu mpaka pale makosa yetu yakithibitishwa ndio tunyooshwe..., ofcourse legally yaliyomkuta Rugemalila sio ubinadamu (hata kama ni fisadi, angekuwa proven guilty haraka kistaarabu then aadhibiwe ipasavyo)...
 
#29October2020; nilimkosoa Sabaya kuhusu kutumia magari yenye namba "feki" za UN kuteka na kuumiza wananchi wa Hai.

#30October2020; Sabaya akanipigia simu mara 3 sikupokea. Akaniandikia sms ya matusi na kutishia kuniua.

#1November2020; Nikascreenshot ujumbe huo na kumtumia rafiki yangu aliyekua kiongozi serikalini, just in case lolote likinitokea.

#26December2020; tukiwa eneo moja Moshi mimi na Don Mbowe, baada ya kuondoka Sabaya alivamia eneo hilo na kudai aoneshwe tulipo. Alipoambiwa tumeondoka alikataa kukubali. Akapiga risasi hewani na kuvuruga biashara eneo hilo.

#28December2020; Akakutana na binamu yangu Moshi (wanafahamiana). Akamwambia mpigie Malisa mwambie aje hapa, lakini usimwambie tupo wote. Jamaa akakataa. Akampiga na kumlaza rumande. Akamnyang'anya simu na hajamrudishia hadi leo.

#13May2021; Mama Samia akamsimamisha kazi kwa tuhuma mbalimbali.

#04June2021; akapandishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Nimwambie nini Mungu?

Malisa GJ
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndiyo unajidanganya hivo?
Jamaa amepakwa mafuta tayar

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
kikosi kazi, kiwa-hasi, pili wapatiwe mashababi wa kuwanyorosha huko nyuma, ndio wasubirie kesi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…