Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, leo Ijumaa, wako mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Bado haijafahamika mashitaka yanayomkabili

=====

UPDATES:

=====

Arusha. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.

CREDIT: Mwananchi

Zaidi, soma: Thread 'Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18' Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Pia soma
1) Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

2) Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

View attachment 1807936
Ole Sabaya akitoka kwenye gari la Polisi akiwa kafungwa PINGU

View attachment 1807996
Ole Sabaya akiwa amechuchumaa mbele ya Mahakama
Muendesha mashitaka ambae ni hakimu anaitwa KWEKA ni mchaga. Awezi akafurukita bwana Sabaya
 
Siku ya leo akipelekwa "GEREZA LA KISONGO" mara baada ya kusomewa mashtaka, mapoloo wa "CHADEMA/ACT" wanamtoa marinda yote 32.

Narudia tena, siku ya leo akipelekwa kisongo, wanamzibua mtaro mapema sana.

Narudia kwa sauti kubwa, watu huko "GEREZA LA KISONGO" wameshaanza shamra shamra za kumpokea "MWALI WAO". Maandalizi yanafanyika huku shangwe ikitamalaki na wafungwa wakijiburudisha na ule wimbo wa "Dada huyooo, kashaolewaaa!!! Na mahaariii, ishatolewaaa!!! mahariiii ishatolewaaaa!!!". Kungwi wa gereza anamsubiri ili amfunde ipasavyo.

● Mungu amlinde Mama Samia, Mungu amlinde Kamanda Salum Hamduni.

● Hatimae tumepata viongozi wanaosimamia "HAKI & UTU", japo hawawezi kutufurahisha raia wote millioni 60, ila mdogo mdogo tutafika.
Maraaaa paaaa kubwa la maadui Bashite nae kashitakiwa anapelekwa gereza la wahuni KEKO. Ni mwendo hulehule hahaha haha hahaha
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, leo Ijumaa, wako mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Bado haijafahamika mashitaka yanayomkabili

=====

UPDATES:

=====

Arusha. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.

CREDIT: Mwananchi

Zaidi, soma: Thread 'Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18' Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Pia soma
1) Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

2) Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

View attachment 1807936
Ole Sabaya akitoka kwenye gari la Polisi akiwa kafungwa PINGU

View attachment 1807996
Ole Sabaya akiwa amechuchumaa mbele ya Mahakama
Clouds TV wamhoji live tena kipenzi chao ili tusikie majigambo yake

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo hoja yako naona kama vile unataka kutuaminisha kuwa mtuhumiwa hatapata haki,kwa vile mwendesha mashtaka ni mchaga...'that's too low'!
Muendesha mashitaka ambae ni hakimu anaitwa KWEKA ni mchaga. Awezi akafurukita bwana Sabaya
 
Atavuna alichokipanda ,kama haki unaona haitotendeke,mpelekee wanasheria bora wa dunia wakamtetee huyo mbakaji.
Hilo ni dili kwa wanasheria wakale mipesa yake ya wizi. Sema wanasheria wakumbuke kutoka fungu la kumi, maana pesa za Moto sana
 
Kwa nini haki asipate apo na wakati ameiba na imethibitishwa au wewe ndio ukumbuki
Exactly...mie sijapinga na haki atapata tu, based on 'ushaidi uliopo' na sio kwa kigezo kuwa mwendesha mashtaka ni kabila fulani, kwa hivyo labda atamwonea kama alivyotaka kusuggest mtoa hoja.... kazi iendelee.
 
Mh lakini hapo utawala wajue huyu pamoja na yote alikuwa kiongozi kwa watu kumtenda hivi mh sijui Kama NI busara
 
1. Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo

2. Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000

3. Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kama sijakosea hayo juu ndiyo madai aliyosomewa Jana na ndio mtoa uzi ameyanukuu kuhusu kujipatia pesa kwa njia za ujambazi halafu gazeti la RAIA MWEMA linasema OLe Sabaya alikutwa na BILIONI TATU benki!!!!

Kumbe kumbe kuwa Bilionea Tanzania rahisi sana!!!
 
Back
Top Bottom