Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Arusha: Mjadala wa Wazi Juu ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania
Wakili Gloria Baltazari, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Bi. Mariam Othman akiwakaribisha na kutoa neno kwa washiriki wa Mjadala wa Wazi Juu ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania unaofanyika jijini DArusha leo tarehe 01/06/2024.
Je umewahi kujiuliza Katiba ni nini? Ina faida gani kwako kama mtanzania wa kawaida? Je umewahi kutamani kutoa maoni ya maboresho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hujapata nafasi?
KATIBA ni mkataba wa kijamii kati wa watawala na wataliwa (Bw. Shilatu). Ni yale yaliyandikwa na ambayo hayakuandikwa ila yanasimamia misingi ya Haki na Utawala bora (Bw. Stolla). Ni Sheria Kuu, kwa sababu inatakiwa kuandaliwa na wenye mamlaka makuu ambao ni Wananchi(Dkt. Mandi)
Tuangazie mkwamo wa Katiba na namna ya kutoka katika mkwamo huo. Ushiriki wa wananchi ukoje katika kutoka katika mkwamo huo na mwenendo wa Taasisi zenye mamlaka katika kuliendela jambo hili.
Pamoja na Sheria kutupatia uhuru wa kujadili namna ya kuboresha Katiba Mpya kuna mambo tumebinywa ikiwemo mjadala usiguse yafuatayo; Urais, Muungano, Uwepo wa Baraza la Mapinduzi, Uwepo wa Serikali ya Zanzibar, Serikali kutokuwa na Dini, Uhuru wa Mahakama, nk.
Tume ya Kuandaa Katiba pia inapewa Immunity inayotunyima uhuru wa kuishurutisha ikiwemo; Huruhusiwi kuishitaki tume hata kama imekosea wakati kikifanya kazi zake.Pendekezo langu Tume pie ishitakiwa iwapo itakosea kisheria.
Katiba ya Tanzania haiwezi kujitetea au kujilinda. Unaweza ukaivunja na ukawa salama. Wakili Matojo Kosata
Mijadala mikubwa kwenye katiba ni minne lakini yote yamejikita kwenye madaraka.
1. Tume ya uchaguzi
2. Muungano
3. Madaraka ya Rais
4. Serikali ya Majimbo
Rais Mstaafu wa @TanganyikaLaw Wakili Francis Stolla amesema sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi haina nguvu ya Kikatiba wakati akiwasilisha mada kwenye mjadala wa wazi juu ya 'Mchakato wa Kupata Katiba Mpya Tanzania' ulioandaliwa na TLS jijini Arusha.
Tuhimize sana katika Elimu ya Uraia na Elimu ya Mpiga Kura. na tume ya Uchaguzi iwe huru ina ifanye kazi yake
Lugha ya Ishara iwe sehemu ya kutoa elimu ya sheria na katiba kwa ujumla. ili na kundi lenye uhitaji pia lifikiwe na kuchangia na kuellewa pia.#KatibaMpyaNiSasa
Mamlaka ya Kuandaa na kuwa na Katiba mpya yako kwa Wananchi. Japo tuiangalie vizuri hii kauli kama ni ya kinadharia ama inaukweli katika utekelezaji wake.
SAUTI ZA WANANCHI MARIDHIANO!
Mimi naiona njia ni feki, mtu akikukosea yeye ndiye anakuomba radhi, sasa wanasiasa wa upinzani utawaona Ikulu wakiyafata maridhiano ni kama wanaenda kuomba radhi kwa kukosewa! Truth, Justice, na Reconsiliation vizingatiwe
Ni uongo kusema tuwaondoe wanasiasa katika mchakato huu wa Katiba Mpya, japo suala hili ni la kikatiba na ni la kisheria, na wananchi ndio wenye power lakini wanansiasa wana mchango mkubwa sana
Wakili Mwandamizi Jijini Arusha Bw. Alute S. Mughwai akitoa mchango wake katika mjadala wa wazi juu ya Mchakato wa kujadili Katiba Mpya ya Tanzania. Amehimiza kupunguza milolongo na kulifanya jambo hili litokee kwani Katiba Mpya ni hitaji la sasa.
"Kwenye Katiba Mpya tuseme mahakama ikishasema sheria ni mbovu basi sheria hiyo ni mbovu hata kama imeshikilia mtu aachiwe" Rais Mstaafu wa @TanganyikaLaw Wakili Francis Stolla.