Pre GE2025 Arusha mjini CCM twende na nani kwenye ubunge 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
2025 iko pale kwenye kona je, wapiga kura wa Arusha mjini tumeshatafakari wa kwenda naye kwenye uchaguzi dhidi ya Godbless Lema. Huko CHADEMA inajulikana kuwa ni mgombea wao wa ubunge ni Lema. Mchakato wao wa kumpata mgombea ubunge huwa ni kiini macho tu. Tayari mgombea wao ni Lema na hata yeye kashathibitisha. Sisi CCM tunafuata sana katiba ya chama chetu kinavyotaka ndo maana hadi muda huu mgombea ubunge hajajulikana.

Mwaka 2020 kwenye kura za maoni walikwepo kina Mrisho Gambo, Philemon Mollel (Monaban) na Alberto Msando. Kwa hali ya kisiasa ilivyo hadi muda huu Gambo na Msando wako active kabisa kwenye siasa. Mbunge viti maalum Catherine Magige naye hayuko nyuma huku Meya wa Jiji Maxmillian naye akizidi kuchanja mbuga. Binafsi nitatoa ushirikiano kwa mgombea yeyote isipokuwa Gambo.
Arusha wakishinda upinzani ni kwa sababu ya migogolo ndani ya CCM Arusha.
 
Lini mnaanza kujiandikisha? Nataka tu ID mimi, kura tutakula mtakazopiga nyie
tusiache kupiga kura hata kama wanaiba tuendelee kupiga kura, kutokwenda ni kuwarahisishia kazi yao haram
 
Whatever it is, havina mchango na personal life langu.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
2025 iko pale kwenye kona je, wapiga kura wa Arusha mjini tumeshatafakari wa kwenda naye kwenye uchaguzi dhidi ya Godbless Lema. Huko CHADEMA inajulikana kuwa ni mgombea wao wa ubunge ni Lema. Mchakato wao wa kumpata mgombea ubunge huwa ni kiini macho tu. Tayari mgombea wao ni Lema na hata yeye kashathibitisha. Sisi CCM tunafuata sana katiba ya chama chetu kinavyotaka ndo maana hadi muda huu mgombea ubunge hajajulikana.

Mwaka 2020 kwenye kura za maoni walikwepo kina Mrisho Gambo, Philemon Mollel (Monaban) na Alberto Msando. Kwa hali ya kisiasa ilivyo hadi muda huu Gambo na Msando wako active kabisa kwenye siasa. Mbunge viti maalum Catherine Magige naye hayuko nyuma huku Meya wa Jiji Maxmillian naye akizidi kuchanja mbuga. Binafsi nitatoa ushirikiano kwa mgombea yeyote isipokuwa Gambo.
Mimi sitatoka ushirikiano kwa Gambo Wala kwa Catherine Magige. Gambo simpi ushirikiano sababu ameumiza watu sana kufikia hapo alipo. Na Catherine simpi ushirikiano sababu hana uwezo... Anakaa bungeni mda mrefu lakini sioni hoja zozote za MAANA alizopeleka kuwasaidia vijana, wanawake na watoto....kule sio jumba la urembo.. halafu alitumiwa cheo chake kufanya fujo msibani. Tutampa yeyote hata kama ni Viola lakini sio kaserini.
 
Arusha haina shida na mgombea kutoka CCM kwani inajiendesha yenyewe .
 
Back
Top Bottom