Uchaguzi 2020 Arusha Mjini: Lema Vs Gambo; Lema atashinda mapema mno

Kwa Tume hii ya uchafuzi, Gambo mapema mshindi.
 
Gambo kusimamishwa kazi siyo kwa bahati mbaya, Gambo hawezi kuchukua fomu ya ubunge ilihali ni RC, kuachishwa kazi ni hatua ya gambo kuweza kuchukua fomu na kuanza kujinadi majukwani. Hata RC wa DSM yapo mawili akachia ngazi au akapewa UBUNGE WA KUTEULIWA HATMAYE UWAZIRI. TRUST ME, THE TIME WILL TELL hahahaaa kiswangilish
 
Anashinda mapemaaa. Watu hawajui siasa za Arusha. CCM wamsimamishe Gambo, anakubalika na wananchi
Wewe ndiyo huzijui siasa za arusha mgoroko, siasa za arusha ni ngumu na rahisi mno!! First and foremost arusha ni anti-CCM,hilo ni la kwanza na la muhimu kuliko mengine,pia arusha wanaweza kukupiga chini huku wanakupenda na kukulilia, Arusha wanaweza kukuchagua huku wakiwa hawakuamini,hawakupendi,wala hawakutegemei uwasaidie,( mf Mh Lema)kumbuka siku ile pale council wananchi walikuwa wakiimba nyimbo za kutokuwa na imani na lema kama hatauza ushindi wake,ila wao wana uhakika kuwa kura walizompigia zinatosha kumpeleka bungeni,wanajua wanachikifanya na pia wanajua matokeo yake!! Ndiyo maana huwezi kuta mwana arusha halisi akilalamika kuwa sijui Lema hajatusaidia hili au lile,zaidi sana utawasoma tu wakina Magonjwa Mtambuka wakimlalamikia kutokea nangulukulu
 
Hizo zote ni kelele, wapiga kura ndo wana maamuzi ya mwisho.
Mtangaza matokeo ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ya nani awe mbunge! Na yeye mwenyewe amevaa jezi ya ccm na kadi yake inaonekana dhahiri kwenye mfuko wa koti lake!! Tusubiri tuone.
 
Cv gambo ilishaharibika labda apewe viti maalumu hawezi shinda Arusha
 
Ushindi wa kura za maoni kwa aliyekuwa Mgombea wa jimbo la Arusha mjini, Mrisho Gambo umezidi kupingwa na makada mbalimbali wa CCM wakiwemo waliokuwa wagombea wenzake wakidai kwamba uligubikwa na rushwa iliyokithiri.

Taarifa zaidi zimeeleza kwamba baadhi ya wajumbe walioshiriki kumpitisha Gambo siku moja kabla walipokea fedha kiasi cha sh 150,000 kila mmoja na hivyo wakati wakiwa katika ukumbi wa uchaguzi tayari walikuwa na mgombea wao mfukoni.

Mmoja wa wajumbe wa uchaguzi huo Peter Mbise kutoka kata ya Lemara alidai kwamba siku moja kabla ya uchaguzi huo Gambo alilala katika hotel ya Mount Meru ili kukutana na wajumbe nyakati za usiku baada ya mazingira ya nyumbani kwake kutokuwa rafiki.

Pia Gambo anadaiwa kufanikisha kulipia ukumbi wa kura katika hotel hiyo jambo lililochangia yeye kujiweka katika mazingira mazuri ya ushindi .

Duru za kisiasa jijini hapa zimedai kwamba iwapo Gambo atapitishwa jimbo la Arusha Mjini litaenda upinzani mapema kwani Gambo hakubaliki kwa wananchi lakini amekuwa akitumia fedha kuwahadaa wananchi ili wamuunge mkono.

Hata hivyo baadhi ya wagombea ambao wamejipanga kutoa malalamiko yao ngazi za juu baada ya kukamilisha kukusanya vielelezo wamedai kwamba msimamizi wa uchaguzi huo, Mary Kisaka amewahujumu kwa kutoonyesha vizuri karatasi ya kura hivyo kujikuta kura zao akipewa Gambo kwani walikuwa haonyeshi ipasavyo karatasi ya kura.

Wafuatao ni baadhi ya makatibu kata wa CCM na viongizi wengine wa CCM waliokuwa wakitumia pikipiki nyakati za usiku kuwakusanya wajumbe na kuwapa fedha, Felix Lemoi mwenyekiti wa CCM kata ya Ngarenaro, Aisha Mbaraka katibu kata Levolosi, Saipuran Rams mwenyekiti UVCCM wilaya ya Arusha.

Wengine ni Juliana Paulo mwenyekiti wa CCM kata ya Sekei, Ally Menu mwenyekiti wa CCM wazazi wilaya, Labora Ndarvoi mwenezi kata ya Themi, Joseph Masawe mwenyekiti wa CCM wilaya, Mary kisaka msimamizi wa uchaguzi na mwenyekiti wa UWT wilaya.

Wengine ni Juma Mohamed katibu wa CCM kata ya Muriet ,Abdi Madava Mwenyekiti wa CCM kata ya Osunyai, Sakina Mpuju Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya, Abraham Mollel (Cobla)mwenezi wa CCM wilaya na Yajaya Njalita mmiliki wa shule ya Green Valley na mbunge viti maalumu aliyemaliza muda wake.

Kwa mujibu wa uongozi wa hotel ya Mount Meru (jina limehifadhiwa) Gambo alitumia chumba namba 403 Gorofa ya NNE kulala katika hotel hiyo kwa siku tatu akikutana na wajumbe .

 
Kwenye ligi kuu kuna timu ikifungwa uwanjani, inatoa malalamiko kutafuta huruma ya alama za kwenye meza..
 
awahonge na wananchi wote wa Arusha ili wampigie kura.
hahaaa!
 
Mnaweweseeka. Mnamfanyia Gambo fitna. Kwa taarifa yenu siamini Kama CCM itasikiliza majungu, na mkumbuke CCM ndo chama kinachoongoza serkali,watafanya uchunguzi na itabainika haya Kama Ni kweli. Mna fitna za kizamani Sana. Na nyie mkiendekezwa ndo mtaleta mpasuko kwenye chama. Acheni unaa
 
Arusha Mjini sioni CCM watampitisha nani......Msando hudhani ana influence kwa watu wengi wa Arusha lakini kiukweli ana influence kwa middle class ambao sio wa piga kura, Mollel anaweza kupata kura kutoka kwa waarusha na wamasai, Gambo sio kama anaweza akaleta upinzani wa maana sana
 
Sema Arusha ina wenyewe, ww huna ulijualo zaidi ya kula bangi na milungi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…