Ushindi wa kura za maoni kwa aliyekuwa Mgombea wa jimbo la Arusha mjini, Mrisho Gambo umezidi kupingwa na makada mbalimbali wa CCM wakiwemo waliokuwa wagombea wenzake wakidai kwamba uligubikwa na rushwa iliyokithiri.
Taarifa zaidi zimeeleza kwamba baadhi ya wajumbe walioshiriki kumpitisha Gambo siku moja kabla walipokea fedha kiasi cha sh 150,000 kila mmoja na hivyo wakati wakiwa katika ukumbi wa uchaguzi tayari walikuwa na mgombea wao mfukoni.
Mmoja wa wajumbe wa uchaguzi huo Peter Mbise kutoka kata ya Lemara alidai kwamba siku moja kabla ya uchaguzi huo Gambo alilala katika hotel ya Mount Meru ili kukutana na wajumbe nyakati za usiku baada ya mazingira ya nyumbani kwake kutokuwa rafiki.
Pia Gambo anadaiwa kufanikisha kulipia ukumbi wa kura katika hotel hiyo jambo lililochangia yeye kujiweka katika mazingira mazuri ya ushindi .
Duru za kisiasa jijini hapa zimedai kwamba iwapo Gambo atapitishwa jimbo la Arusha Mjini litaenda upinzani mapema kwani Gambo hakubaliki kwa wananchi lakini amekuwa akitumia fedha kuwahadaa wananchi ili wamuunge mkono.
Hata hivyo baadhi ya wagombea ambao wamejipanga kutoa malalamiko yao ngazi za juu baada ya kukamilisha kukusanya vielelezo wamedai kwamba msimamizi wa uchaguzi huo, Mary Kisaka amewahujumu kwa kutoonyesha vizuri karatasi ya kura hivyo kujikuta kura zao akipewa Gambo kwani walikuwa haonyeshi ipasavyo karatasi ya kura.
Wafuatao ni baadhi ya makatibu kata wa CCM na viongizi wengine wa CCM waliokuwa wakitumia pikipiki nyakati za usiku kuwakusanya wajumbe na kuwapa fedha, Felix Lemoi mwenyekiti wa CCM kata ya Ngarenaro, Aisha Mbaraka katibu kata Levolosi, Saipuran Rams mwenyekiti UVCCM wilaya ya Arusha.
Wengine ni Juliana Paulo mwenyekiti wa CCM kata ya Sekei, Ally Menu mwenyekiti wa CCM wazazi wilaya, Labora Ndarvoi mwenezi kata ya Themi, Joseph Masawe mwenyekiti wa CCM wilaya, Mary kisaka msimamizi wa uchaguzi na mwenyekiti wa UWT wilaya.
Wengine ni Juma Mohamed katibu wa CCM kata ya Muriet ,Abdi Madava Mwenyekiti wa CCM kata ya Osunyai, Sakina Mpuju Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya, Abraham Mollel (Cobla)mwenezi wa CCM wilaya na Yajaya Njalita mmiliki wa shule ya Green Valley na mbunge viti maalumu aliyemaliza muda wake.
Kwa mujibu wa uongozi wa hotel ya Mount Meru (jina limehifadhiwa) Gambo alitumia chumba namba 403 Gorofa ya NNE kulala katika hotel hiyo kwa siku tatu akikutana na wajumbe .