Arusha: Mke ampa kipigo mumewe hadi kumuua

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Bandambili kata ya Sombetini jijini Arusha anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kumpiga mume wake hadi kuua.

Mwanaume huyo ajulikanae kwa jina la Daudi ambae ni fundi ujenzi alifariki dunia usiku baada ya kupewa kipigo usiku mzima na mkewe huyo wa ndoa aliezaa nae watoto kadhaa.

Majirani wamesema ni kweli mwanaume huyo hupigwa mara kwa mara na mkewe pamoja na kusachiwa hela mfukoni mkewe kwa kushirikiana na watoto.

Soma Pia: Arusha: Auwawa kwa kupigwa na kitu kizito baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake

Wazazi wa marehemu Daudi wamesema kuwa ni kwa muda mrefu kijana wake amekuwa akipigwa na huyo mwanamke na kurudi nyumbani anauguzwa akipona anarudi tena kwa mwanamke huyo na hata wao wazazi wakienda polisi kijana wao anaenda polisi na kusema kuwa amemsamehe mkewe.

Wazazi wa daudi wanasema hali hiyo imekuwa ikijirudia mara nyingi kupigwa na kujeruhiwa na mkewe hadi mauti yalipomkuta.
 
RIP mwamba!najua uwezo wa kumpiga na kummumiza mke wako ulikua nao!lakini utayari wa kupigana na mwanamke sio kila mwanamme anao!

Mara nyingi tunaepusha shari na kuondoka nyumbani au kwenda Kwa michepuko kupoza hasira coz ukimuua mwanamke nani atalea watoto!!?na sisi me kipawa Cha kulea watoto hatuna!!

RIP CHIEF
 
Mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Bandambili kata ya Sombetini jijini Arusha anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kumpiga mume wake hadi kuua.

Mwanaume huyo ajulikanae kwa jina la Daudi ambae ni fundi ujenzi alifariki dunia usiku baada ya kupewa kipigo usiku mzima na mkewe huyo wa ndoa aliezaa nae watoto kadhaa.

Majirani wamesema ni kweli mwanaume huyo hupigwa mara kwa mara na mkewe pamoja na kusachiwa hela mfukoni mkewe kwa kushirikiana na watoto.

Soma Pia: Arusha: Auwawa kwa kupigwa na kitu kizito baada ya kuingilia ugomvi wa mtu na mpenzi wake

Wazazi wa marehemu Daudi wamesema kuwa ni kwa muda mrefu kijana wake amekuwa akipigwa na huyo mwanamke na kurudi nyumbani anauguzwa akipona anarudi tena kwa mwanamke huyo na hata wao wazazi wakienda polisi kijana wao anaenda polisi na kusema kuwa amemsamehe mkewe.

Wazazi wa daudi wanasema hali hiyo imekuwa ikijirudia mara nyingi kupigwa na kujeruhiwa na mkewe hadi mauti yalipomkuta.

Wamem'bamanda DAUDI mpaka ameresiti ini pisi
 
Back
Top Bottom