Arusha: Mke wa Mtu auawa na mchepuko wake baada ya kutoa mimba ya mchepuko

Arusha: Mke wa Mtu auawa na mchepuko wake baada ya kutoa mimba ya mchepuko

Kukosekana uaminifu kwenye ndoa ndio chanzo cha mambo mengi ya hovyo sana kwenye mahusiano,yaani mtu unamtumia mke wa mtu mpaka unamuona ni mali yako unaweza kumfanya chochote unachotaka......
 
Tena wamsokomeze miti kabisa shenzi huyu 🤬
Mimi nadhani hapa mume wa marehemu ndio anatakiwa kuchunguzwa, yaani unaamini kuwa anaweza kuwa alikuwa amekaa tu anaacha mkewe ana mwanaume mwingine na kila mtu anajua... Uweze kano mkubwa ametekeleza haya mauaji, akaacha viatu na na nguo za hawara wa mkewe hapo ili jamaa apate msala. Ila kwa polisi wetu wanaweza kufikia conclusion kwa kukuta tu viatu na nguo za hawara hapo.
 
622d0291c01bc3e7f561d6ff12538bc2

MWILI wa mwanamke aliyetambulika kwa jina la Teddy Mallya mkazi wa Ilboru Kisiwani, Arumeru mkoani Arusha umekutwa umetupwa kwenye shamba la migomba akiwa mtupu na baadhi ya majeraha mwilini ikiwemo ya kung’atwa na meno huku akidaiwa kuuawa na hawara yake (mchepuko).

Mwili huo ulipatikana jana majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya wapita njia kuuona na kutoa taarifa. Taarifa za wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa marehemu alikua na uhusiano wa siri na mwanaume nje ya ndoa ambaye anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana na kumtuhumu marehemu kuwa alitoa ujauzito wake.

Mume wa marehemu, Richard Lanyuni alisema mkewe alikuwa mfanyabiashara wa pombe za kienyeji aina ya mbege, hakuonekana kurejea nyumbani muda wa kawaida na ilipotimu majira ya saa saba usiku niliamua kulala ndipo kesho yake alipata taarifa za kuuawa.

“Kuhusu mke wangu kuwa na uhusiano na mwanaume huyo siwezi kujua ila hakuwa na ujauzito. Naomba vipimo vya kitaalamu vifanyike kujua kama kweli alikuwa na ujauzito maana ana shughuli zake mimi siwezi kumchunguza sana,” alisema Richard.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alisema jeshi linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumuua mwanamke huyo, na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wamtaa wa Ilkiroriki, Emmanuel Lazaro, mtuhumiwa anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu na alikamatwa kutokana na baadhi ya nguo zake na viatu kukutwa eneo la tukio.
Jamii yetu ina mbilinge nyingi sana
 
Mwenzio akinyolewa we tia maji ajali umkumba yeyeto tu uwe smart usiwe smart,wake zetu ni michepuko ya wengine.
 
Back
Top Bottom