Arusha: Mkuu wa wilaya amtuhumu Mbunge kuhamasisha maandamano

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felisian Mtehengerwa amesema kitendo cha wafanyabiashara wadogo (Machinga) katika jiji la Arusha kuandamana usiku kinachochewa na wanasiasa wenye nia ovu ya kuihujumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na amemtuhumu mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kuwa kinara wa mpango huo haramu kwa kisingizio cha kubughudhiwa na Migambo wa jiji.

Akiongea na vyombo vya habari na kutokea ufafanuzi madai hayo ,Mtehengerwa alidai kuwa Jambo hilo linaratibiwa na kuchochewa na wanasiasa kwa lengo la kuichafua serikali na kuwachonganisha wafanyabiashara hao na serikali yao.

Alidai upo ushahidi kwamba Gambo amewapeleka baadhi ya viongozi wa machinga bungeni dodoma kwa lengo la kuwachongea viongozi wa mkoa ili waonekani hawafai kwa kisingizio cha migambo kutesa machinga kwa kipigo

Alimtaka Gambo kuacha siasa za maji Taka kwani uongozi wote wa mkoa unajua jinsi anavyo hujumu kwa kutumia majukwaa ya kisiasa

"Jana usiku Machinga wameandamana katika katakana ya jiji la Arusha wakidai mwenzao Isaac Sangwa ameuawa kwa kupigo cha Migambo huu ni uzushi na ni mpango mchafu unaochochewa na wanasiasa wachache kwa maslahi yao ili kumhujumu rais Samia Suluhu ,wasitake kutulazimisha tutumie mamlaka yetu tulionayo "

Alisema wao kama viongozi hawawezi kuruhusu Machinga kufanya biashara kiholela wakati walishatengewa maeneo yao .

"Hili ni jiji la utalii hatuwezi kuruhusu Machinga afanyebiashara kiholela hii ni kufukuza watalii kwa sababu ya wanasiasa uchwara wanaoendesha siasa za maji Taka kusaka umaarufu "

Awali wamachinga wa soko la Kilombero jijini hapa, waliandamana wakiwa na madai mbalimbali ya kunyanyaswa kwa kipigo,kuombwa rushwa ya ngono na pesa na Migambo wa jiji la Arusha.

"Naitwa Janet Lema huyo kijana Isack ni mmachinga mwenzetu alichukuliwa na migambo na kupigwa vibaya sana na hatujui yupo wapi tumekuwa tukinyanyasika kwa kipigo na kuombwa rushwa ya ngono na pesa
 
Aise kwahy dc unajipendekeza kwa mh rais na sio wananch wenzako ooh nilisahau kumbe umeteuliwa na rahis, aya muache gambo awe mtetez mana ndie alichaguliwa na hao wananch
 
Hii mbona haifanani kabisa na watu waliokuwa na hasira au watu wanaoandamana
Screenshot_20230430_105614_WhatsApp.jpg=w352-h180-p-k-no-nu
..... Ukisema wanaselebuka? Haya.
 
Hilo Jimbo limeshawashinda linamsubiri God bless Lema.
Huyo Lema ndio kila siku alikuwa anaitisha maanadamano mpaka waendesha watalii wakawa wanapita njia za vichochoroni na ukumbi wa AICC ukafungwa ukajengwa JNICC.

Madhara ya Lema.

Huyo DC ndio kama jiji limemshinda. Akae chini na viongozi wenzie waangalie changamoto na namna ya kuzitatua.kinachoonekana ye na Gambo wanavimbiana vifua.

Ndio maana dc kamuunganisha samia. Kila analosema anasema Gambo anataka kumchonganisha samia na wananchi.
 
Dc simamia sheria na kanuni za mipango miji waitake kuturudisdha enzi za mwendazake jiji la Arusha lilikuwa km kambi ya wakimbizi. Barabara zote za katikati mwa jiji maeneo ya soko kuu yaani mtaa wa kati zilifungwa zote, kuanzia chini ya mti mpaka stand kuu ata kwa miguu ilikuwa hupiti, bado frind's kona. Kuanzia mianzini mpaka stand kuu ni vibanda si juu ya mitaro si mbele ya maduka ya watu. Tusirudi kule hao machinga wamepangiwa maeneo yao wasitake kutuletea ushamba wao kule walikotokea, ni watu wamezoea uchafu, kubanana.

Watu wasitumie umachinga kuharibu ustaarabu km wameshindwa ustaarabu wa jijini warudi walikotokea siyo lazima wabanane mjini hata kulima ni kazi. Gambo mwambieni aanze kuaga, ni mtu fulani mwenye roho isiyoridhika, anataka awe mbunge wakati huohuo anataka awe RC, amewachnganya sana watu wa Arusha tangia akiwa mkuu wa Mkoa ndio maana stand mpya ya bondeni haijajengwa mpaka leo. Azingatie mipaka ya madaraka yake. Km vipi DC mpige ndani 48 hours ashike adabu, kuwa mbunge siyo uvuruge amani, utulivu na usalama wa eneo lenye utawala halali.
 
Hilo Jimbo limeshawashinda linamsubiri God bless Lema.
Lema akagombea kwao uchagani, Lema hawezi kurudi Arusha hatujasahau alivyouletea mji wa Arusha umaskini, wanacnhi walikuwa hawana muda wa kufanya kazi ni mikutano, maandamano kila mara. Kuna watu wazuri watajitokeza muda ukifika.
 
Lakini wote ni watoto wa mama mmoja wataelewana tu.
 
Lema akagombea kwao uchagani, Lema hawezi kurudi Arusha hatujasahau alivyouletea mji wa Arusha umaskini, wanacnhi walikuwa hawana muda wa kufanya kazi ni mikutano, maandamano kila mara. Kuna watu wazuri watajitokeza muda ukifika.
Iwapo Uchaguzi utakuwa HURU na wa HAKI jiandaeni kukabidhi JIMBO.

In Polepole's voice.
 
Hili swala la Wamachinga likiachwa hivi hibi kisiasa huko mbeleeni itakuja kuwa balaa tupu,
 
Ndio gharama za kuteua watoto kuongoza watu, anachojua yeye ni kutafuta mtu wa kumtupia lawama kwake huo ndio utatuzi wa tatizo..mji mkubwa kama huu anapewa amature kuongoza, so tu mzaha ni dharau kubwa kwa wana-arusha, mambo ni hivi hivi sehemu zingine, hivi hakuna watz watu wazima over 50 wenye sifa za kuongoza?
 
Katoto kadogo kanatawala ARUSHA hako ka DC. Ni fedheha kwa CCM na serikali
 
Ndio gharama za kuteua watoto kuongoza watu, anachojua yeye ni kutafuta mtu wa kumtupia lawama kwake huo ndio utatuzi wa tatizo..mji mkubwa kama huu anapewa amature kuongoza, so tu mzaha ni dharau kubwa kwa wana-arusha, mambo ni hivi hivi sehemu zingine, hivi hakuna watz watu wazima over 50 wenye sifa za kuongoza?
Mama yetu hana Imani na wazee, ilihali yeye mwenyewe ZEE
 
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felisian Mtehengerwa amesema kitendo cha wafanyabiashara wadogo (Machinga) katika jiji la Arusha kuandamana usiku kinachochewa na wanasiasa wenye nia ovu ya kuihujumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na amemtuhumu mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kuwa kinara wa mpango huo haramu kwa kisingizio cha kubughudhiwa na Migambo wa jiji.

Akiongea na vyombo vya habari na kutokea ufafanuzi madai hayo ,Mtehengerwa alidai kuwa Jambo hilo linaratibiwa na kuchochewa na wanasiasa kwa lengo la kuichafua serikali na kuwachonganisha wafanyabiashara hao na serikali yao.

Alidai upo ushahidi kwamba Gambo amewapeleka baadhi ya viongozi wa machinga bungeni dodoma kwa lengo la kuwachongea viongozi wa mkoa ili waonekani hawafai kwa kisingizio cha migambo kutesa machinga kwa kipigo

Alimtaka Gambo kuacha siasa za maji Taka kwani uongozi wote wa mkoa unajua jinsi anavyo hujumu kwa kutumia majukwaa ya kisiasa

"Jana usiku Machinga wameandamana katika katakana ya jiji la Arusha wakidai mwenzao Isaac Sangwa ameuawa kwa kupigo cha Migambo huu ni uzushi na ni mpango mchafu unaochochewa na wanasiasa wachache kwa maslahi yao ili kumhujumu rais Samia Suluhu ,wasitake kutulazimisha tutumie mamlaka yetu tulionayo "

Alisema wao kama viongozi hawawezi kuruhusu Machinga kufanya biashara kiholela wakati walishatengewa maeneo yao .

"Hili ni jiji la utalii hatuwezi kuruhusu Machinga afanyebiashara kiholela hii ni kufukuza watalii kwa sababu ya wanasiasa uchwara wanaoendesha siasa za maji Taka kusaka umaarufu "

Awali wamachinga wa soko la Kilombero jijini hapa, waliandamana wakiwa na madai mbalimbali ya kunyanyaswa kwa kipigo,kuombwa rushwa ya ngono na pesa na Migambo wa jiji la Arusha.

"Naitwa Janet Lema huyo kijana Isack ni mmachinga mwenzetu alichukuliwa na migambo na kupigwa vibaya sana na hatujui yupo wapi tumekuwa tukinyanyasika kwa kipigo na kuombwa rushwa ya ngono na pesa
Acha wauwane!! Ila mwenyew kasharudi!!
 
Naona unajaribu kumlinda sana mlinda legacy mwenzako, kijana gambo!!

Back
Top Bottom