mkuu kanisa katoliki lina mabingwa wa kuongoza saikolojia ya waumini wao na hata wale wasio waumini wao.
shughuli zozote zile za uuzaji bidhaa au huduma huitwa masoko.shughuli za marketing hujumuisha kutafuta mahala pa kuuzia bidhaa au huduma zako na kutafuta wateja.
umuhimu wa masoko katika biashara yako,ni sawa na umuhimu wa moyo katika kiwiliwili cha mwanadamu.moyo unaposimama mapigo,uhai hutoweka.basi vivyo hivyo shughuli za masoko zinaposimama biashara hufifia na hatimaye kufa kabisa.
mfano,usipofungua biashara yako au ukifungua bila muda maalum wateja watapotea na hatimae biashara yako itakufa.unaweza ukamwangalia kakobe kabla na sasa alikuwaje.
katika biashara,kila mtu anaweza kuwa mteja wako siku moja lakini si lazima kila mtu awe mteja wako.kwa hiyo ni muhimu ujue mteja wako ni nani!
unaweza kujua mteja wako ni nani kwa kujua mtu fulani anataka nini! kumbuka kuwa mteja hununua bidhaa au huduma ili kutimiza mahitaji au matakwa yake na si yako.kanisa katoliki ililiona hili hivyo kuweka dini pekee isingeleta ushawishi kwa watu bila kuweka vivutio vitakavyosababisha watu kushawishika navyo.
kwa hiyo ili ufanikiwe katika biashara yako, ni vema kujua kwa nini na kwa 7bu gani mteja ananunua bidhaa au huduma yako,ama sivyo utashindwa kulenga na kutosheleza mahitaji yake.