Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
. Moto uliowaka kwa siku tano mfululizo katika nyumba iliyopo Kijiji cha Olovolosi wilayani Arumeru umesababisha wapangaji kulala nje ili kuokoa maisha yao.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Emmanuel Losiyoni amesema moto huo ulianza Julai 7 na unaunguza nguo, magodoro na vyombo vya ndani tu.
"Baada ya moto kuanza ilidhaniwa ni hitilafu ya umeme lakini ulipozimwa na umeme kukatwa bado unaendelea kuwaka na kuunguza vitu kutoka chomba kimoja hadi kingine," amesema Losiyoni.
Nyumba hiyo inayomilikiwa na mama mmoja maarufu kama Mama Mudi ambaye amehamia mkoani Tanga ina vyumba 14 vya wapangaji.
"Wapangaji wanaona moto unawaka kuanzia sebuleni kwenye vyombo na kufuata nguo na licha ya kuzimwa umekuwa ukiwaka tena," amesema.
Kutokana na utata wa moto huo, amesema ameagiza wapangaji kuhama kwenye nyumba hiyo ili kuokoa maisha yao na ameripoti polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuangalia namna ya kuwasaidia.
Mmoja wa wapangaji, Rehema Peter anasema wanahisi moto huo unasababishwa na mambo ya kishirikina na tayari wapangaji saba wamehama.
"Kama tumezima umeme na hakuna anayepika ndani kwa nini moto unajitokeza mara kwa mara?" amehoji Rehema.
Joel Gidioni, jirani na nyumba hiyo yenye moto wa ajabu anasema umewaka mara tano na mwisho ilikuwa jana usiku hali ambayo imezua taharuki.
"Naona wapangaji wanahama kuokoa maisha yao. Hili ni jambo la ajabu na halijawahi kutokea," anasema.
Mwananchi