Arusha: Mtandao wa kuteka, kubaka, kupora wanawake maarufu waanza kudakwa

Arusha: Mtandao wa kuteka, kubaka, kupora wanawake maarufu waanza kudakwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa ni viongozi wa mtandao wa utekaji, uporaji na ubakaji wa wanawake maarufu jijini hapo.

RPC wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kuongeza kuna wengine wawili wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo.

Inaelezwa kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia gari dogo kuwateka wanawake kwa kuwafuna kitambaa usoni, kuwapeleka wanapotaka, kuwapora fedha na mali kisha kuwatupa

Wamekuwa wakiifanya tabia hiyo kwa kuwatongoza wanawake katika kumbi za starehe au hoteli kubwa

Polisi wanaendelea na msako wa mtandao huo, hivyo hawawezi kuwataja majina kwa sasa kwa kuwa inaweza kuharibu uchunguzi.

Inadaiwa kuna kesi zaidi ya 20 katika Kituo Kikuu cha Arusha, pia baada ya kukamatwa walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na kukutwa na vitu vingi vita thamani ikiwemo cheni za dhahabu, saa na thamani mbalimbali.


Chanzo: SimuliziNaSauti
 
Back
Top Bottom