Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Breaking News: Mwandishi wa Habari Mkoani Arusha, Lilian Oddo ambaye anafanya kazi na mwandishi wa Wasafi tv Bw. profit Mmanga, na yeye amekamatwa akiwa maeneo ya darajani/vibandani njia ya kwenda Kwa Morombo Jijini Arusha, na amepakiwa kwenye gari nyeusi ambayo ndani yake yupo Profit, bado haijulikani wamepelekwa wapi.
===================
Arusha: Mwandishi Lilian Oddo Hajulikani Alipo
Taarifa kutoka Mkoani Arusha inadaiwa Mwandishi wa Habari, Lilian Oddo hajulikani alipo.
Lilian anayefanya kazi kwa ukaribu na mwandishi wa Wasafi TV, Potte Mmanga ambaye naye alichukuliwa na watu wasiojulikana mapema Juni 15, 2022, inadaiwa amechukuliwa na watu wanaodhaniwa ni walewale waliomchukua Potte.
Taarifa za awali zinaeleza Lilian alichukuliwa akiwa maeneo ya Darajani/Vibandani njia ya kwenda Kwa Morombo. Taarifa zaidi zitafuata, vyombo vya usalama havijapatikana kuzungumzia taarifa hizo.
Pia soma: Mwandishi wa Habari wa Wasafi Media - Arusha, Potte Mmanga adaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana
Chanzo: Gadi TV