Arusha: Polisi auawa kwa panga akijaribu kumkamata mwizi usiku nyumbani kwake

Mnasema ndo taaluma ya uandishi lakini naona inachosha kukirudia kichwa cha habari mara nne kwenye habri moja. Kahabari kafupi lakini maandishi ni mengi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo polisi alienda peke yake kumkamata mhalifu saa 5 usiku ?!
 
Wameru noma sana....
 
Huyu kajitakia utaendaje kukamata mtuhumiwa peke yako tena saa tano usiku ni uzembe..
 
Fake story. Mtu kauwawa wanashindwa vipi kutaja jina lake wala kuonyesha picha yake. Jambazi na yeye jina lake linahifadhiwa ili iweje?
 
Saa tano usiku , peke yake anavizia mtaani, je kama alikuwa anavizia mke wa mtu? Maana askari hawachelewi kugeuza kesi.

Mie mtuhumiwa wa kwanza ni huyo aliyeripoti wizi wa mazao yawezekana huyo ndio aliyengeneza mtego mzima. Njagu kajipeleka akajikuta ameingia mtegoni.

Pamoja sifurahii kifo Ila polisi wajifunze kuishi na watu, hilo panga wangekatwa wote wanaobambikizia watu kesi
 
Sijawahi kuelewa wala kuamini statements za mapolisi[emoji848]
 
Halafu utasikia nyumbu mmoja anasema kwanini jambazi fulani alietwangwa risasi hajakamatwa afikishwe mahakamani!
Statement za polisi huwa zina ukakasi

Na we umeamini kabisa kilichoelezwa hapo?
 
huyo alifumaniwa sema wameamua watuzuge ki’hivo.

we unaendaje kukamata mwizi usiku wa saa 5 usiku peke yako ?

ila hata hivo nikisikia polisi amepatwa na lolote baya hua nafurahi maana hawana roho ya utu hao jamaa
 
Hilo ni GENGE LA POLISI CCM yaani lilikwenda kwenye ugoni haya likazikwe tu hakuna namna
 
Good angemchoma na moto kabisa ili kupoteza ushahidi.


Kutokuwa na shule bwana! utaendaje kukamata mwizi usiku ukiwa mwenyewe?

Huyu alienda kuomba rushwa bila shaka!!

Pole pole Karma!

Rekebisha title. Kauwawa na sio Kaua
 
Kwa maelezo haya inaonyesha hakukuwa na tukio la kiaskari katika kutekeleza majukumu yake,inawezekana ni ugomvi binafsi au tukio la kufumaniana.Iweje jina la mtuhumiwa lifichwe? Kwa nini aende pekeake kumkamata mharifu usiku saa tano?mwenyekiti wa mtaa/kijiji alikuwa wapi?vipi auawe na jirani kwa panga na si mtuhumiwa mwenyewe? kuna maelezo mengi hayajakaa sawa kwa taarifa hii ufafanuzi wahitajika zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…