Kamanda wa Polisi Mkoa, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amethibitisha tukio hilo leo Septemba 11, 2022 na kueleza kuwa wanamshikilia Allen Wilbard Kasamu, dereva wa Lori la mafuta lililotumika kusafirisha Mirungi
Kamanda Masejo amesema wamewakamata pia watuhumiwa wengine 38 wanaohusishwa matukio tofauti ya uhalifu kwenye operesheni iliyofanyika kwa siku tano kuanzia Septemba 5 hadi 10,2022
Ametaja vitu vilivyokamatwa kuwa ni pamoja na Pikipiki 13 zinahusishwa na ushiriki wa matukio ya uhalifu, lita 4 za Gongo, Lilo 70 za Bangi na Laptop 3.