Arusha: Polisi, Walimu na Wanafunzi kuanzisha club za kupambana na uhalifu shuleni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkaguzi wa kata ya Mkundi Mkoani Morogoro Mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Anna Manumbu amebainisha kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana walimu na wanafunzi wanaunda club za kupambana na uhalifu mashuleni ambazo zitaongeza kasi ya kupambana na uhalifu na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Mkaguzi huyo amebainisha endapo club za kupambana ana uhalifu mashule zikiimarishwa mashuleni zitaibua taarifa nyingi za uhalifu wanaofanyiwa baadhi ya wanafunzi katika kata hiyo.


Pia amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kuondoa changamoto ya kupata taarifa sahihi pindi changamoto inapotokea ya uhalifu na unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa baadhi ya wanafunzi katika eneo hilo la kata ya Mkundi wilaya Morogoro Mjini Mkoani Morogoro.

Mbali na hilo amewataka walimu kutengenezea mahusiano mazuri na kubadilishana taarifa kutoka kwa wananfunzi, wazazi na walezi wa wanafunzi hao ili kupata taarifa sahihi pindi wanafunzi hao wanapopata changamoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…