Arusha: Polisi waua majambazi watano. RC Gambo atoa pongezi

Arusha: Polisi waua majambazi watano. RC Gambo atoa pongezi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1580380266845.png

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shanna amesema kikosi cha jeshi la polisi Mkoani humo kimewaua majambazi sugu watano wakati wakijibizana risasi na polisi na kuwakuta na silaha aina ya Shotgun Pump Action 32265,Chinese Pistol,Bastola 1 bandia,risasi 11 pamoja na simu 2 & pikipiki 3.

Kamanda Shanna amesema msako unaoendeshwa na Jeshi la Polisi hautaishia hapo, na watahakikisha kuwa tabia za kuvuna pasipo kupanda zinazofanywa na vikundi vya watu wachache ndani ya mkoa huo zinadhibitiwa.

Amesisitiza kuwa jiji la Arusha litakuwa shwari, na akionya kuwa wale wote wanaofanya vitendo vya uhalifu wataangukia mikononi mwa Polisi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama katika jiji hilo. Pia amechukua nafasi hiyo kutuma salamu na kumpongeza Waziri mpya wa Mambo ya ndani Mhe. George Simbachawene kwa kuanza kazi vizuri.

"Sisi kama mkoa tutashirikiana na Wizara yake ya Mambo ya Ndani kuona namna ya kuwapa zawadi Askari hawa waliyofanikisha jambo hili (la kuwaua majambazi sugu 5) maana wamenifanya niwe na furaha sana". Amesema RC Gambo.
 
Hii taarifa mbona haijakamilika? Hao wajambazi wameuwawa lini, Arusha sehemu gani na walikuwa wanafanya tukio gani au polisi waliwezaje kuwagundua kuwa ni majambazi (leads/intel).

Isijekuwa ni kiki.
Mkuu siku zote nikisikia taarifa za namna hii huwa najiuliza maswali kama uliyouliza, watu wengi sana wanauawa kwenye mazingira kama haya bila hatia yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii taarifa mbona haijakamilika? Hao wajambazi wameuwawa lini, Arusha sehemu gani na walikuwa wanafanya tukio gani au polisi waliwezaje kuwagundua kuwa ni majambazi (leads/intel).

Isijekuwa ni kiki.

Hilo ndilo swali la muhimu. Mtu anatoa taarifa kama alikuwa anakimbizwa vile.
 
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwauwa majambazi sugu watano waliokuwa na silaha za moto katika majibizano makali ya risasi wakati wakielekea kufanya uhalifu wilayani simanjiro.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha,Kamanda wajeshi la polisi mkoani hapa,Jonathan Shanna amesema kuwa,tukio hilo limetokea Jana januari 29 mwaka huu majira ya saa 3:45 usiku katika njia panda ya Mateves katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kamanda Shana alisema kuwa,tukio hili limetokea baada ya jeshi la polisi kupata taarifa za kiintelijesia kuwa majambazi hao walikuwa wamepanga kwenda kufanya tukio la ujambazi katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Alisema kuwa, majambazi hayo walipanga kutumia barabara ya Afrika Mashariki (Bypass) kupitia Olasiti Hadi mzunguko wa kwa mrombo kwa kutumia usafiri wa pikipiki tatu ambazo walikuwa nazo.

Amesema kuwa, Mara baada ya polisi kupata taarifa hizo waliweka mtego katika njia panda ya Mateves ambapo ilipofika majira ya saa 3:45 usiku Askari hao waliona pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatokea upande wake Mateves kuelekea barabara mpya ya Afrika Mashariki, ambapo walisimamishwa na Askari hao lakini badala ya kutii amri majambazi hayo walianza kufyetua risasi.

Ameongeza kuwa,baada ya hapo ndipo kikosi kilianza kujibu mapigo ambapo majibizano hayo yalichukua muda takriban dakika 35 , ambapo majambazi wanne walifariki hapo hapo huku jambazi mwingine Mmoja aliyekuwa nyuma aligeuza na pikipiki yake na kukimbia umbali was mita 500 lakini naye alipigwa risasi na kudondoka.

Aidha katika eneo la tukio walikuta vitu mbalimbali vilivyokuwa vinatumuwa na majambazi hao ikiwemo pikipiki tatu ambazo ni MC 871 BWR aina ya Skygo ,MC 555 CGE aina ya Kinglion, MC 478 AYV aina ya Toyo,bunduki moja aina ya Shortgun pump action yenye namba 32265, Chinese Pistol moja iliyofutwa namba zake za usajili, bastola moja ya bandia.

Alitaja vitu vingine kuwa ni magazine mbili za Chinese ,Pistol moja ikiwa na risasi 8 na nyingine ikiwa na risasi 1, maganda 7 ya risasi ya Chinese Pistol, risasi 2 za bunduki aina ya Shortgun, maganda 5 ya risasi ya Shortgun na simu mbili aina ya Tecno na moja aina ya Oking.

Aidha alisema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa bunduki hiyo aina ya Shortgun pump Action iliibiwa januari 26,mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku nyumbajni kwa Jackson Msangi baada ya majambazi hao kuvunja nyumba yake iliyopo maeneo ya Burka, kata ya Olasiti.

Amesema kuwa, walifanikiwa pia kuiba simu ya mkewe aitwaye Nikira Msangi ambapo yet na mume wake wametambua bunduki na simu vilivyoibiwa siku hiyo waliyovamiwa.

Aidha miili ya marehemu imehifadhiwa ktika hospitaliti ya mkoa ya Mount meru kwa uchunguzi wa Daktari na utambuzi.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amelipongeza jeshi hilo kwa kazi nzuri ya kufanikisha kuwashibiti na hatimaye kuwaua majambazi hao kwani wangeweza kusababisha madhara makubwa kwa askaro au huko walipopangiwa kwenda kufanya uhalifu.

Gambo amesema kuwa, usalama ni kipaumbele chetu na mkoa wa Arusha ni mkoa wa kitalii kwani asilimia 25 ya fedha zinazopatikana zinatokana na utalii, hivyo kuna haja kubwa ya kuimarisha ulinzi kuhakikisha watalii wanakuwa salama muda wote.
IMG-20200130-WA0008.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom