ArD67
JF-Expert Member
- Nov 14, 2016
- 2,817
- 2,044
Katiba ya JMT inajieleza wazi nini maana ya Tanzania, nani na wapi na ni lini walikuja kutubadilishia hiyo katiba ituoneshe Arusha kuwa sio Tanzania? Au unadhani sote ni vilaza humu?Huyo uliyemnukuu ni nani na ni raia wapi? Bila shaka sio mtanzania, tena alitakiwa akamatwe haraka sana baada ya kutoa kauli hiyo bila kujali alimaanisha nini. Kila mtu anajua tumetoa sehemu ili kuweka ofisi za EAC, kwahiyo vikao vinaishia kwenye hizo ofisi tu wasilete upumbavu, mambo ya Arusha ni ya watanzania.
Namaanisha, kwa muktadha wowote ule labda uwe wa dhahania, Arusha ni Tanzania. Raia wa kigeni watafika hapo kama wageni na si vinginevyo.