Arusha: Sita wafariki ajali ya Lori, Noah

Arusha: Sita wafariki ajali ya Lori, Noah

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya gari baada ya Toyota Noah kugongana na Lori aina ya Scania katika eneo la Alkatani, Kata ya Sepeko, Tarafa ya Kisongo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo Aprili 20, 2022.

Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Arusha – Babati, RPC wa Arusha, Justine Masejo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Lori aliyeshindwa kulimudu gari na kuhamia upande mwingine, ambapo anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

“Lori lilikuwa likitokea maeneo ya Makuyuni, Noah ilikuwa ikitokea Arusha Mjini, majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Jeshi iliyopo Monduli, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Maunti Meru.

“Hatujafahamu majina kamili ya watu waliopoteza maisha, uchunguzi unaendelea,” - RPC wa Arusha, Justine Masejo.

noah.jpg
lori.jpg

 
Watu sita wamefariki na wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Alkatani, Monduli mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo ikihusisha Noah na lori (Scania).

Polisi wanamshikilia dereva wa lori hilo baada ya uchunguzi wa awali kuonesha uzembe wake ndio chanzo cha ajali hiyo.


noah.jpg
lori.jpg
 
Haya malori mbona yanasababisha sana ajali hao madereva wana shida gani!
RIP kwa wote waliotangulia mbele ya haki na majeruhi wote wapate quick recovery, tusikimbilie kwenye majibu rahisi, tatizo kubwa barabara zetu bado zipo duni mno, finyu mno,na magari mengi hayana sifa za kuwa barabarani
 
Haya malori mbona yanasababisha sana ajali hao madereva wana shida gani!
Magari mabovu, madereva waliochoka/hawana uzoefu, miundombinu ya barabara mibovu, rushwa. Ukijumlisha vyote hivyo kwa pamoja lazima kuwe na shida na hii na kwa malori na magari ya aina nyingine.
 
Watu sita akiwemo dereva wa gari wamepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika ajali iliyotokea wilayani Monduli, Mkoani Arusha .


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ,Justini Masejo tukio hilo lilitokea Jana majira ya Saa nne usiku katika kijiji cha Alikatani,wilayani humo.


Kamanda alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noar lenye namba T 186 DFY ambalo liligongana uso kwa uso na Lori aina ya Scania namba T 250 CA .


Alifafanua kwamba gari aina ya Scania lilikuwa likitokea Eneo la Makuyuni Kuelekea jijini Arusha huku gari aina ya Noar likitokea Arusha mjini na kuelekea Wilayani Karatu likiwa limebeba abiria.


Kamanda alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado haijajulikana Ila wapo katika hatua za uchunguzi wa tukio.


"Taarifa za awali zinaonesha kuwa dereva wa Lori ambaye anashikiliwa na Polisi alihama ghafla kutoka upande wake na kwenda upande wa pili na kukutana na gari aina ya Noar" alisema.


Alisema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya Mkoa Mount Meru na majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospital ya jeshi iliyopo wilayani humo.


Kamanda Masejo alitoa rai kwa madereva wa magari kuwa makini wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto ikiwemo kuzingatia kanuni za usalama barabarani.








 
Dah poleni sana huko Arusha ndugu na jamaa...Malaulau na madera wa Noah poleni sana kwa msiba
 
Mmoja kati ya waliofariki ni mjomba wangu, ajali inaumiza sana.
 
Back
Top Bottom