Arusha Technical College kufuta mahafali kisa wahitimu kugoma kukodisha majoho

Arusha Technical College kufuta mahafali kisa wahitimu kugoma kukodisha majoho

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Ni habari iliyotikisa wengi, wengine wakacheka kwa uchungu na wengine wakashika vichwa: Chuo cha Arusha Technical College (ATC) kimetangaza kuwa hakutakuwa na sherehe za mahafali kwa wahitimu wa mwaka 2025, zilizopangwa kufanyika tarehe 31 Januari 2026.
1769715640886.jpg

Sababu? Asilimia 7 tu ya wahitimu ndio waliolipia na kuchukua majoho ya mahafali. Kwa mantiki ya chuo, idadi hiyo ni ndogo kiasi cha kufanya sherehe “kutokuwa na tija kiuchumi na kiutawala.”
images (100).jpeg

Hapo ndipo maswali mazito yanapoanza. Tangu lini mahafali yakawa mradi wa kiuchumi? Je, shahada sasa inapimwa kwa faida na hasara kama biashara ya mkaa au mazao sokoni? Au labda kuna somo jipya chuoni: Graduation Economics 101?
1769715204338.jpg

Kwa miaka yote, mahafali yamekuwa ishara ya mwisho wa safari ndefu ya kitaaluma—furaha ya wazazi, fahari ya wahitimu, na kumbukumbu kwa chuo chenyewe. Sio tukio la kutafuta faida, bali la kutimiza wajibu wa taasisi kwa wanafunzi wake. Je, kama wahitimu wangekuja bila majoho lakini na tabasamu, sherehe ingekuwa batili?
images - 2026-01-29T224552.182.jpeg

Uamuzi huu unaacha dukuduku: kuna uhusiano gani wa moja kwa moja kati ya uchumi wa chuo na sherehe za wahitimu? Je, chuo kinategemea mapato ya majoho kuendesha shughuli zake? Kama ndivyo, basi kuna shida kubwa kuliko mahafali yaliyofutwa.
1769715204338.jpg

Na hapa ndipo lawama zinapoelekezwa kwa uongozi. Mkuu wa chuo, mzee wetu Dr. Musa Chacha, katika hili umefeli balaa. Sio kwa kufuta sherehe tu, bali kwa ujumbe unaotumwa: kwamba heshima ya wahitimu inapimwa kwa malipo yao. Katika nchi ambayo elimu inapiganiwa kwa jasho na machozi, kauli hii ni kama chumvi kwenye kidonda.
images (100).jpeg

Mahafali si biashara. Ni heshima kubwa. Na ni heshima, hata ikikosa majoho, haipaswi kufutwa.
 
Pameqnza kuchangamka sasa wafute tu watupe vyeti vyetu tukaweke kabatini tuingie kitaa kusaka life kazi zenyewe ziko wapi mpaka nigaramie joho na sina uhakika wa ajira
Kweli kabsq
 
Degree zenyewe hizi za Google, kufanya sherehe ni kupoteza rasilimali fedha.

Natoa pongezi kwa ambao hawakutoa hio michango.

Sababu ambazo chuo kimetoa ni evidence kuwa sherehe hazikuwa na tija yoyote kwa wahitimu ila walikuwa wanafaidisha Chuo.

Kichwa kisicho na akili, ni adhabu kwa Miguu.
 
Watu 844 hawataki mahafali
Kwa mtizamo wangu hali ya kiuchumi mbaya
Pia naomba Wengine amabao nmepata bahati ya Kusoma nje hivi mlikuwa mnalipa pesa ya Joho??
Mimi binafsi nchi nlosoma majoho ni bure
 
Watu 844 hawataki mahafali
Kwa mtizamo wangu hali ya kiuchumi mbaya
Pia naomba Wengine amabao nmepata bahati ya Kusoma nje hivi mlikuwa mnalipa pesa ya Joho??
Mimi binafsi nchi nlosoma majoho ni bure
Kwa Arusha Technical College wao mahafali ni tija ya kiuchumi Mkuu
 
Wanafunzi wa hovyo kbs, anyway shauri Yao haituhusu na umaskini wao.
 
Back
Top Bottom