BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi Ungalimited Jiji la Arusha wamelazimika kukaa chini kutokana na uhaba wa madawati huku uongozi ukidai ni kutokana na ukarabati wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika shule hiyo kongwe.
Hata hivyo Ofisa Elimu Msingi Jiji la Arusha,Hosseni Madengale amesema kunaukarabati unaoendelea wa vyumba vya madarasa huku madawati yaliendelea kuwekwa alama kwaajili ya kupelekwa madarasi
Mwandishi wa habari hii alifika shuleni hapo na alishuhudia baadhi ya wanafunzi hao kukaa chini kwenye sakafu na wengine matofari wakiwa wamechafuka vumbi ,huku walimu wakiendelea kufundisha na walimu wengine wakirudishia milango kukwepa kamera za mwandishi wa habari.
Kubainika kwa hali hiyo kumebukiwa na walezi na wazazi, baada watoto wao kurejea majumbani wakiwa wamechafuka vumbi mithiri ya kibega wa mifuko ya saruji wakati shule hiyo ipo katikati ya Jiji la Arusha na baada ya wazi kuwahoji walidai wanakaa chini tangu shule zifunguliwe .
"Sisi kama wazazi hii hali ya watoto wetu kukaa chini darasani hatujaipenda kabisa mtoto anakuja nyumbani amechafuka ,mgongo unamuuma kwa kukaa ameinama rora waseme tuchangie madawati kuliko hii hali "alisema mzazi Joha Maliwa.
Baadhi ya wanafunzi walishuhudiwa wakiwa darasani wengine wamekaa kwenye madawati na wengine wanakaa chini wakiandika notisi za masomo katika madaftari yao wakiwa wameweka madaftari kwenye mapaja Yao.
Baada ya mwandishi kujionea hali halisi shuleni hapo,Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi,Emmanuel Kileo alisema hakuna mwanafunzi anakaa chini bali kunaukarabati unaoendelea na madawati yanawekewa namba ili yaingizwe madarasani
"Hakuna mwanafunzi anayekaa chini bali kunaukarabati unaendelea na hela ziliingia kwakuchelewa lakini watoto wanasoma kama kawaida isipokuwa darasa la pili wanaingia saa 5 asubuhi na kutoka saa nane mchana ila tunaendelea na ukarabati wa vyumba vya madarasa"
Naye Ofisa Elimu Msingi Jiji la Arusha,Madengale alipopigiwa simu ili kudhibitisha madai hayo alisema amefika shuleni hapo na kujionea hali halisi ya ukarabati hivyo aliisisitiza hakuna mwanafunzi anayekaa chini.
Alipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kupitia kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Hargeney Chitukuro kutenga fedha za mapato ya ndani sh,milioni 20 kwaajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa vitano vya madarasa.
Naye Diwani wa Kata ya Ungalimited, Mahamoud Omari alisema shule hiyo ni shule kongwe iliyokuwa ikihitaji ukarabati mkubwa na kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwa wavumilivu wakati ukarabati huo ukiendelea kwani hivi sasa wamepokea sh,milioni 20 na badae zitaongezeka kwaajili ya ukarabati wa shule hiyo kongwe ya Ungalimited.
"Ni aibu kwa shule za mjini kuingia darasani kuona shule inavuja,ukarabati unaofanyika sio mdogo awali tulikuwa tunapokea fedha ndogo kwaajili ya ukarabati wa shule hii lakini hivi tutaendelea kuikarabati kadri fedha zitakapoongezwa "
Chanzo: a24habari.blogspot