DOKEZO Arusha: Wananchi wa mtaa wa Mirungi wasambaza vipeperushi mtaani kupinga uuzaji wa mirungi kama mchicha sokoni

DOKEZO Arusha: Wananchi wa mtaa wa Mirungi wasambaza vipeperushi mtaani kupinga uuzaji wa mirungi kama mchicha sokoni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wananchi wa kata ya Osunyai mtaa wa Ngusero wilaya ya Arusha jijini hapa wameungana kwa pamoja na kuchapisha vipeperushi mtaani vinavyoeleza kuchoshwa na uuzwaji wa madawa ya kulevya aina ya mirungi kama ilivyo mboga sokoni.

Vijana wa boda boda wamekuwa wakiingia na kutoka katika baadhi ya nyumba katika mtaa huo huku wakiwa wamebeba mafurushi makubwa ya mirungi na wengine wakiwa wanauza hapo hapo mtaani kama vile mchicha sokoni bila bughdha yoyote toka kwa uongozi wa mtaa na polisi.

Wananchi hao wamefikia uamuzi huo baada ya viongozi wa mtaa pamoja na polisi kushindwa kudhibiti hali hiyo kwa muda mrefu sasa na hivo mtaa wao kuitwa mtaa wa Mirungi.

Wananchi hao wamesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona hata watoto wao na familia zao zikijiingiza katika matumizi mabaya ya madawa.
 
Ukishatafuna hiyo mimi huwezi kunitafuna.

Maana hata ukinyanyuka hausimami!
 
Juzi mmepigiwa sala mixer dua
La watu wa dini zote labda itasaidia

Ova
 
Back
Top Bottom