Arusha: Wananchi waomba kujengewa daraja

Arusha: Wananchi waomba kujengewa daraja

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wananchi wa kata ya sinoni na Themi katika halmashauri ya jiji la Arusha, wameiomba serikali kuwajengea daraja linalounganisha Kata ya Themi na Sinoni kutokana na Kuwa ni miaka zaidi ya mitano sasa imepita tangu kuvunjika kwa daraja la awali lilokuwepo.

Wakazi hao Wamekuwa wakipata shida wakati wa kwenda na kurudi kazini wakati wa kuvuka mto huo unaotenganisha kata hizo mbili kwa kukosa daraja. Na katika kipindi cha mvua hali huwa mbaya zaidi kutokana na kufurika kwa mto.

Baadhi ya vijana wa boda boda wanaopaki jirani na mto huo wamesema kuwa Kukosekana kwa daraja hilo hata kwa upande wao pia ni tatizo kutokana na kwamba miundombinu ya mto huo ulivyo ni ngumu kwa pikipiki zao kuvusha abiria kutoka kata moja kwenda nyingine.

Hivyo basi uwepo wa daraja ingekuwa kiunganishi muhimu cha uchumi wa wananchi wa kata zote mbili,na pia kurahisisha shughuli nyingine za kiuchumi na maendeleo kufanyika kwa urahisi .

IMG-20230108-WA0012.jpg
IMG-20230108-WA0012.jpg

IMG-20211113-WA0063.jpg

IMG-20230108-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom