Arusha: Watendaji wa kata, kijiji wasimamishwa kazi, kupisha uchunguzi

Arusha: Watendaji wa kata, kijiji wasimamishwa kazi, kupisha uchunguzi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Idd Hassan Kimanta amewasimamisha kazi Mtendaji Kijiji na kata ya Mwandeti na Afisa Tarafa ya Mukrati kuwa chini ya ungalizi ili kupisha uchunguzi zaidi na hatua kali zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao kazi kati ya Mkuu wa Mkoa na maafisa tarafa Watatu wa halmashauri ya Meru, watendaji wa kata 26 na vijiji 90 pamoja na wakuu wa idara na vitengo katika halmashauri hiyo.

Aidha Kimanta alisema kuna uzembe mkubwa umefanyika katika utendaji wa majukumu yao, hasa kushindwa kudhibiti kilimo cha bangi katika maeneo yao.

“Haingii akilini bangi inalimwa kwa miezi 3 na mwezi wa 4 inavunwa wewe mtendaji wa kata na kijiji upo hapo na hauchukui hatua yoyote”.

Alisema haieleweki kwanini nyie kama viongozi mmeshindwa kudhibiti kilimo cha bangi kwa muda wote huo na mpo hapohapo.

Aliwataka watumishi kuacha kufanyakazi kwa mazoea kwani dhama hizi ninza kuwajibika kila mtu kwenye nafasi yake.

Kimanta alisisitiza zaidi kwa viongozi wa kata na vijiji kuwafichua wote wanaolima bangi katika maeneo yao badala ya kuwaficha, amesema kwa kufanya hivyo wanachangia kuiharibu jamii.

Aliwataka viongozi hao wa kata na vijiji kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hivyo watakuwa wamewatumika vyema wananchi wao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Arumeru Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro, alisema tatizo kubwa kwa watumishi wa wilaya hiyo ni kufanya kazi kwa mazoea ndio maana wanashindwa kuchukua hatua mbalimbali za kiutendaji katika maeneo yao.

Aidha, Muro aliwataka watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wawe wabunifu zaidi katika kutekeleza majukumu yao badala ya kuwasubiria viongozi wa ngazi ya juu tu.

Kimanta amefanya ziara fupi katika wilaya ya Arumeru, baada ya maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli dhidi ya tuhuma za ulimaji bangi katika wilaya hiyo
 
Haya kazi njema, kila la heri wakukada
 
Rc hajui historia ya hiyo bangi huko juu,Hiyo bangi hata ukiikata leo mvua zikanyesha inaota tena.

Aulize waliomtangulia wamwambie,ndio maana kila mwaka baada ya msimu wa mvua miez michache baadae unaona kuna bangi inateketezwa huko orkokola au Pengine..
 
Angemsimamisha na Mkuu wa Wilaya, haiwezekani bangi ikalimwa kwa miezi mitatu ndani ya Wilaya yake, na mwezi wa nne ikavunwa, DC asiwe na taarifa au asichukue hatua
Hapo inge make sense zaidi
 
Kunya anye bata akinya kuku shiida.
Serikali inapokwepa kuboresha maslahi watumishi hukaa kimya but mtumishi anapokwepa wajibu wake huwajibishwa
 
Mwenyekiti wa Kijiji hajui na yupo,afisa kilimo hajui na yupo?,wananchi wa kijiji wajui na wapo kijiji hicho?!!!
Mwisho wa siku ni utafutaji wa sifa za kiutendaji bila kutafuta suluhu ya Kilimo cha bangi.
Viongozi wafanye utafiti kwanza ili wafahamu ,zao hilo soko lake lipo wapi,na matumizi ya zao lenyewe ijulikane.

Kama wananchi watashirikishwa,ufumbuzi utapatikana!!!

Kama bangi ina soko,wakulima waruhusiwe walime ili wajiongezee kipato,kama ni dawa ilimwe ili isaidie katika tiba stahili.
 
Iddi umeanza Kwan speed utafika mwisho?
 
ila mi naona bangi ingehalalishwa tu maana mi sioni madhara ya bangi kwa kweli...
 
Angemsimamisha na Mkuu wa Wilaya, haiwezekani bangi ikalimwa kwa miezi mitatu ndani ya Wilaya yake, na mwezi wa nne ikavunwa, DC asiwe na taarifa au asichukue hatua
Upo sawa kwani yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama. Kwa nafasi Yake hiyo alichukua hatua zipi? Ang'olewe kwa kushindwa kutumia mamlaka na vyombo vya dola anavyovisimamia!
 
Angemsimamisha na Mkuu wa Wilaya, haiwezekani bangi ikalimwa kwa miezi mitatu ndani ya Wilaya yake, na mwezi wa nne ikavunwa, DC asiwe na taarifa au asichukue hatua

Dc ndo aliyemtonya mkuu wa kitengo nchini na kukamata huo mzigo.
 
Back
Top Bottom