Hilo darasa hamna asiye jua umuhimu wa kodi nchi hii, pia hiyo hiyo taasisi inaweza kuwa fimbo kuonea watu.Wengine tunashindwa kuchangia mada za humu sababu wachangiaji wanachangia kwa mihemuko ya kisiasa.
Mimi ni mtaalamu wa kodi. Ngoja nikupe darasa kidogo kama utaweza kunivumilia kuandika kidogokidogo.
Charitable
...Ni kweli Mkuu. Hata kwa kuangalia hizo picha zao tu hapo. Hapana Mzazi Masikini hapo, kwa maana halisi ya neno ' Masikini'.Tatizo lingine katika hizo shule vigisuvigisu ni vyingi sana kwa watoto kupata nafasi katika shule hizo. Wengi wa watoto wanaosoma huko wazazi wao au walezi wao wanakipato kizuri tu, ila zinaitwa shule za watoto wa masikini.
Wewe sema ukweli kwamba walifanya makosa ya kutofuata sheria acha kukurupuka hadi unakosea.Kama mnavyoona kwenye mitandao ya wassap, TRA inefreeze account za shule za st Jude kwa kisingizio kuwa wamekuwa hawalipi kodi wakati wanasomesah watoti wa Kitanzania bure kabisa kwani Gharama zote na Mishahara ya Walimu imekiwa ikilipwa na serikali ya Austria kama ufadhili.Chanzo cha kazi hii nikwamba wakati wa kampeni serikali ya mkoa na wilaya iliiomba shule itoe magari ili waweze kusomba wapambe wake lakini shule ikasema wao lama NGO hawaruhusiwili kisheria kuegemea chama chochote cha siasa..Sasa kwa kuwa kijani wako madarakani wameamua kuanza nal kuwa wanakwepa kodi hivyo shule ifilisiwe na watoto elf 1 inabidi warudi kwao nawafanyakazi zaidi ya 300 kukoswa ajira.Je TRA kwa hili anafanya haki.?je wanmkomoa nani?
Mfano mzuri Sana. Watu hawaelewi hiliHiyo shule haiwezi kusajiliwa kama charitable Organisation sababu haina sifa za kuwa charitable. Hivi shishi food ya Shilole inauza chakula kwa rate za market value, halafu atokee Mo Dewji aseme naomba uwe unawalisha kituo cha watoto maskini na wasiojiweza halafu Mo dewji anakulipa kwa rate ileile unayowachaji watu wengine, utasema shishi food inafanya charity?
Hawa ndio wazazi Maskini waofadhiliwa?Wazazi Maskini zaidi ya 2000 ambao watoto wao wanafadhiliwa kimasomo katika shule ya St. Jude iliyopo Arumeru Mkoa wa Arusha, wameandamana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakitaka shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ifunguliwe ili Watoto wao waliosimamishwa masomo kwa zaidi ya wiki mbili waweze kuendelea na masomo.
Wazazi hao wamedai kwamba mamlaka ya mapato Tanzania TRA imekausha akaunti yao kwa kuchota fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwa madai kwamba shule hiyo haijalipa kodi ya Serikali kwa muda mrefu na hivyo uongozi wa shule hiyo kulazimika kuwasimamisha masomo Wanafunzi kwa kushindwa kujiendesha baada ya fedha zilizopo kwenye akaunti kuchukuliwa na TRA.
====
Arusha. Wazazi zaidi ya 1,000 wa wanafunzi wanaopatiwa ufadhili wa masomo katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya St. Jude iliyopo Arumeru mkoani Arusha, wameandamana hadi ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kulalamikia hatua ya watoto wao kusitishiwa masomo kinyume na utaratibu.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba mosi, 2020 wazazi hao waliituhumu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani hapa kufungia akaunti za mfadhili wao, jambo lililosababisha shule kushindwa kujiendesha ikiwemo kuwahudumia watoto.
Salma Mohamed na Latifa Jafari, wakazi wa jijini hapa wamesema katika kipindi cha wiki mbili watoto wao wamesimamishwa masomo kwa madai shule inadaiwa, hivyo kuiomba Serikali kuwaruhusu kuendelea na masomo.
Wazazi hao pia wanaituhumu TRA kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti ya shule na kusababisha kushindwa kujiendesha.
Akizungumzia tuhuma hizo, meneja wa TRA mkoa wa Arusha, John Mwigura alikiri kuidai kodi ya muda mrefu shule hiyo, lakini St Jude ilikataa deni hilo kwa madai haifanyi biashara, hivyo haiwezi kulipa kodi na kukimbilia ngazi mbalimbali ikiwemo Mahakama ya Rufaa kupinga tuzo la kodi akibainisha kuwa mahakamani TRA ilishinda kesi hiyo na St Jude iliamuliwa kulipa kodi hiyo.
View attachment 1638958View attachment 1638959
Hapa kuna school fees ambayo inalipwa na wafadhili au mfadhili, hivyo hiyo school fees inayolipwa na mfadhili ni mapato kwa ShuleNilikuwepo kwenye hyo misa
Vicar General alisema shule inategemea mapato yake kutoka kw wafadhili wa Australia. Na hakuna mwanafunzi anaelipa ada, ni kwa ajili tu ya kusaidia watoto wanaotoka familia za kipato cha chini
Asa sijui kwa nn hadi misaada inatozwa kodi, wakati hamna faida wanayopata
Kweli tupuHiyo picha haina mtu maskin hata mmoja
Lipeni Kodi ya serikaliMkuu wewe tulia shule ya kata mpeleke mwanao na nduguzo.
Kwa hiyo yale Magari yanayo park St Joseph Cathedral Dsm ni ya Kanisa Katoliki?? Au Magari yanayo park ksnisa la kilutheri hapo Arusha mjini ni ya KanisaAngalia Fanya tafiti hata Magari yao yanapack wapi hapa mjini kama siyo st Theresa Cathedral usibishe usiyojua.
Tanzania elimu ni bure sasa, hao kwanini waende kwenye hiyo shule , wakiendelea na ukaidi majengo yatapigwa bei
Sasa wewe umepewa mpaka kesi ya 2012 , lakini wewe na akili yako bado unashadadia siasa za Mwaka huuHilo darasa hamna asiye jua umuhimu wa kodi nchi hii, pia hiyo hiyo taasisi inaweza kuwa fimbo kuonea watu.
Mimi nasema jinsi issue ya siasa ilivochochea kukomoana, tena juzi tu before uchaguzi ilikuwa Moto sasa imetoka juzi hii.Sasa wewe umepewa mpaka kesi ya 2012 , lakini wewe na akili yako bado unashadadia siasa za Mwaka huu
Wanakoromea nyumbani