Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Hadi ana migodi
Sio mgodi ni migodi...jamaa yupo vizuri
 
Hiki ni baadhi ya kisa chake, tumeshuhudia pia akidharau kazi za bodaboda na mengi tu, angelikaa miaka 10 sijui ingelikuwaje?
IMG_20230304_104530_988.jpg
 
Ulitaka hawa vijana wawe vibaka? Ulitaka wafanye kazi gani?

Leo hii Africa nzima boda boda ni usafiri unaosaidia watu na kutoa ajira pia. Hii ni sababu hata mazingira ya uchumi yako rafiki kwa watumiaji.

Wewe kuishi Canada kwa ukimbizi uchwara ndio unadhania kila nchi ina mazingira sawa kama ya Canada? Hufai kuwa hata Mbunge.
 
Wewe ujui siasa ilivyo ndio maana siasa waliita ni mchezo mchafu kwasababu wanasiasa hawaaminiki Lema si ndio huyo huyo akisema Lowassa ni fisadi na Ndio miongoni mwa mtu aliyempokea chamani na kumpigia kampeni ya Uraisi kama aliongea haya mimi ni nani niamini maneno yake
Hakuna mfuasi wa awamu ya tano anaekubali kua upinzani hasa CDM waliuawa, waliteketwa, waliteswa, kupewa kesi fake, wala halihitaji evidence bali wasiojua mamb bali ni mashabiki watakwambia ulete evidence!!
 
Godbless Lema amewatukana vijana Waliojiajiri kwa kuwaambia wanafanya kazi za laana, hii suala limeacha simanzi kwa vijana wengi sana.

Jana nilikua Arusha nimezunguka sehemu mbalimbali kuona wamepokeaje kauli hii yenye dharau kubwa sana. Hakika walio wengi wanajuta kwa Nini walienda Kumpokea Lema.

Serikali inapambana usiku na mchana ili vijana wapate ajira na wajiajiri alafu leo lema anakuja kuwatukana?

Lema anapaswa kuomba radhi kwa kauli hii. Yeye kwa kuwa anakula na kulala bure kule canada basi anataka watu wote waishi hivyo kitu ambacho hakiwezekani. Imeandikwa kwenye vitabu takatifu kuwa mwanaume atakula kwa jasho, wewe inakuaje unakula bure alafu unaleta dharau kwa wanaokula kwa jasho?

Lema anapaswa kuomba radhi mara moja kwa kauli hii.
Lema yupo sahihi kabisa, bodaboda sio ajira kwa sababu hakuna mtu ambaye alienda shule ili aje kuwa dereva bodaboda ✋🏽
 
Lema imekuwaje? Mbona kama vile kawa kichaa?
lazma ukweli usemwe,
enzi za yule baraghuli magufuli alitesa watu sana, hasa wa kaskazini walinyanyasika sana.
wamenyang'anywa mali na pesa, aliwatumia kina sabaya.
 
Lema muongo kama alikuwa anakwenda kukagua migodi yake kwa kuvaa baibui, ukafikiri Serikali aina watu wake huko kwenye migodi? Serikali ikikutaka hata uchimbe shimo inakukuta huko kwenye shimo, Serikali kama ilikuwa inamwitaji hatawakati wa kuvuka mpaka angelikamatwa tu, mbona Nyarandu alirudishwa na akuna kilichompata!na mpaka Sasahivi yuko ccm anakula bata; Chadema uongo wanaotunga kuaribu sifa za Magufuli utawarudia tu, hauwezi kupanda kwa kukanyaga mtu au kimchafua ukadhani wewe utakuwa salama.Akuna jipya ambalo Magufuli alitenda ambalo watangulizi wake hawakuwai kulitenda.
Well, now naona tumekubaliana juu ya uhalifu waliofanyiwa upinzani awamu ya tano na umekubaliana kua haikuanzia awamu ya tano!! Hapa sasa tunaenda saw 🙌🙌!! Kuhusu ukwepaji kwa serikali kuna raia weng walikwepa serikali lkn miaka mbeleni ndipo wakaja kamatwa, imagine kiwanda kinaiibia serikali umeme kwa zaid ya miaka kadhaa je serikali haikuepo? Sio kila wahujum wanakamatwa on time mengine huchukua muda!!
 
Mwenye akili hawezi shabikia kikoba eti kinasaidia
Wanataka kumdumaza maskini akili aweke hela kwenye kibubu au ndoo wao waweke zao benk
Nikweli vikoba ni umaskini mzunguko wa pesa umekuwa mdogo matokeo yake tunaishi kwa kukopa huko mtaani kuna taasisi nyingi za kukopesha wamegundua biashara hiyo inalipa sana, jamii mfu ambayo haiwezi kubuni njia sahihi za kuwezesha kuinua kipato cha mtu mmojammoja inaishia kwenye mikopo inayoitwa kausha damu
 
Punguza akili kuganda!! Kila jambo lina conclusion zake kweny vyombo husika!! Acheni waseme waliyopitia ili nafsi zao ziridhike, mnaumia juu ya wao kusema wengi wenu ni wahusika wa mauaji na utekaji!!
Kila mtu akisema yanayomuuma si tutageuza taifa kuwa kituo cha maombolezo. Tangu huyo lema afike siskii sera yoyote aliyosema zaidi ya kashfa tu! Kwa mtaji huo 2025 wataendelea kuwa wapiga debe
 
Godbless Lema tangu arudi ametoa kauli zilizoibua mijadala, hisia nyingi sana na tafsiri za kila aina kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii.

Amezungumza kuhusu uduni wa ajira za bodaboda na VICOBA visivyo na maana yoyote kwenye jamii ambapo yeye anasema hivi vitu ni "urasimishaji wa umaskini' unaofanywa na watawala. Ameongelea pia hadaa za nabii mkuu Geor Davie wa huko Arusha.

Amegusa vijana, wanawake na dini ambayo ni makundi makubwa sana ya mtaji katika siasa za nchi hii. Japo yote aliyoongelea ndio ukweli mtupu lakini chama chake pia bado kina malengo ya kushika dola hivyo bado kinayahitaji sana haya makundi yote.

Tanzania anayoitazama lema ni ile ya kisasa iliyoendelea, yenye maendeleo ya watu na vitu ambayo raia wake wengi wana ishi hadhi ya binadamu wa karne ya 21. Kwa bahati mbaya sana hatujaifikia hiyo Tanzania na hivyo Lema anapaswa kukubaliana na hali halisi ya sasa tu.

Kama yeye na chama chake wanataka kushika madaraka siasa wanazopaswa kufanya ni zile zile za kijanja janja za kuwahadi bodaboda, mama ntilie, wamachinga na makundi ya dini kwamba watawatengenezea mazingira mazuri zaidi ya kufanya kazi zao na kushamiri. Wenye nguvu katika chama kwa "maslahi ya chama na kushika dola" waafikiane naye asiongele mambo ya gigabyte(GB) katika bongo za watu zinazoweza kuhimili Megabyte(MB) tu.
 
Kwa hiyo hapa Tanzania Kuna upungufu wa ma operator wa matrekta si ndio? Hiyo unayoita kazi ya kula imewawezesha kuanzisha miradi Mingi tuu

nisome mstari kwa mstari utanielewa vizuri sana, lengo langu sio kuwadharau au kuwakejeli bali lengo ni kuhakikisha Taifa linanufaika moja kwa moja na kwa kiasi kikubwa na nguvu kazi hasa ya vijana.

Vijana wenye nguvu ndio msingi wa ujenzi wa Taifa, kuchezea hii nguvu kazi ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom