Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Katika maelezo yote ni kwamba Lema anaulalamikia Umaskini ulioletwa na CCM lakini anaogopa kuitaja CCM na kujificha kwenye Kichaka cha Magufuli

Ni kweli nchi yetu ina umaskini na Ndio sababu Shujaa Magufuli alipigana hadi mwisho wa uhai wake ili aongoze ukombozi

Lema kaikimbizia familia yake Canada kwa sababu ya Umaskini na Ndio sababu anasema haitarudi

Sasa Chadema itueleze itatukwamuaje katika huu umaskini Bila ya wao Kulamba Asali

Mungu awabariki
 
Tanzania haiwezi kuwa labda baada ya miaka mia mingine
 
Usiitazame Tanzania kwa filling za ulaya utaonekana unaendeshwa na ganja Tanzania Bado hatuwezi kufanya mambo kwa kulinganisha na Dubai
 
Inawezekana unasema kweli lkn huenda wenzetu huko walikuwa wanafanya hizo kazi za ovyo lkn walikuwa na mikakati yakujiondoa walipokuwa na Sasa wamefanikiwa labda uniambie kama ccm inahuo mkakati/mpango wakuvuka hapo

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Yaani huyo marehemu kuiba Hela za watu ndio alikuwa anapambana na umaskini?

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Ni mjinga tu ndio ataona Lema amekosea..
kwa nini kuna western countries na third world countries?
Western countries sababu kodi za wananchi zitatumika ipasavyo. Miundo mbinu ni kipaumbele. Usafiri wa public ni wa uhakika.. sasa huku kwetu usafiri wa bodaboda ndio tunajivuninia.. Hakuna ajira kwa sababu ya uzembe wa viongozi…

Yes bodaboda ni laana.. Watawala wajifambue waache matumizi mabovu ya pesa za wenyewe….

Ajira ndio wimbo Mkuu kwa vijana sio bodaboda…

Nchi ina resources za kutosha lakini hakuna ajira kutwa kukopa…
Watawala hawasikii
Kuna nadini kuna vyakula kuna vyanzo vya maji kuna ardhi nzuri kuna vivutio vya wataliii lakini ni maskini wa kutupwa…

Lema yupo sahihi … read between the lines utamwelewa. Kaza ubongo uelewe anamaanisha nini.

Lema kanyaga twende.. Ukweli mchungu
 
Hapana hapana nyinyi wenyewe chadema Kila mnakoenda mnategemea hao hao boda boda huwezi kuwaita bodaboda ni laana sio kweli ,,yeye mwenyewe lema hapo kabla alikuwa anafanya kazi Gani ? Kazi za viwandani zinamshahara wa shilingi ngapi? Unewahi kujua Hilo? Mm nawajua watu wa bodaboda ambao Leo wamejenga nyumba zao na wanamaisha pia TU !! Unataka serikali iajiri watu milioni 60? Huko america Kuna omba omba na wengine wanalala kwenye makorido lakini Kuna madereva bodaboda kabisa kwenye majimbo yote ya marekani usitumie siasa kutweza utu wawatu!
 
Siasa za chadema always wamezoea kutukana serikali lakini kwakua ameona Rais Samia Suluhu ameikomboa nchi amerejesha amani na democrasia pamoja na uhuru wa kuongea ameona hawezi kumtukana badala yake amehamia kutukana watanzania hakika ametuvunja moyoi sana
 
Hivi neno," NITAKUKOLIMBA" lilitokana na nini hasa!!!
 
Kombora limetuwa kunako bravo Nabii

Mtaji wenu ni kuwafanya watu wawe maskini ....sasa imebumburuka
 
Walala hoi na wenye kipato cha kati ndio wengi nchini, wote hawa wana laana??? Acha siasa kwani wenye laana hawatakupigia kura. Hama nchi iliyolaaniwa uende Canada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…