Lema sijui ana elimu ya kiwango gani?, sidhani kama unaweza zungumza hayo ukiwa umefundwa vyema na wazazi wako.
1. huwezi kubeza jitihada za mwingine ktk kutafuta riziki ili naye aishi, bodaboda wanafanya mambo mengi sana hapa nchini, wanalipa kodi, wanasaidia ndugu zao, wanaendesha maisha ya familia zao, wanajiajiri kupunguza vibaka mtaani...wanafanyika baraka kwa watu wengine wanaowazunguka hasa katika kutoa huduma.
2. Nabii huyo hata kama hafanyi kazi kwa kumfurahisha mtu hapa duniani, ila inaonyesha ana upendo kiasi fulani hata kama ni wa kinafki ila anao kwa kuwasaidia wengine, ndio maana hapa duniani hatufanani..mawazo ya lema si mawazo ya nabii, kila mtu afanye lile analolimudu, kama ni kanisa atalijenga na si kwa mapenzi ya lema. 😀 😀