Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Wafanyabiashara Soko la Samunge wasema Lema hawamtaki
Mwaka 1995 wananchi wa Karatu hawakuwa na tatizo lolote dhidi ya CCM ila waliamua kukiadhibu chama baada ya kukata jina la Wilbroad Slaa waliyemtaka na kurudisha jina la Patrick Qorro ambaye alikuwa mbunge kwa miaka mingi. Enzi za mwalimu Nyerere pia wananchi walimchagua mgonbea binafsi na kumkataa mgombea aliyependwa na Mwalimu Nyerere. 2025 upinzani unaweza kushinda saa tatu asubuhi endapo Gambo atarudishwa kugombea. Ubaya wa Gambo ni kuwavuruga hadi CCM wenzake. Na kwa siasa za Arusha zilivyo huwa ni sekunde kadhaa tu wanaCCM kusapoti kina Lema. CCM isirudie makosa.
 
Linapokuja suala la kumpinga Nabii feki Geor Davie ninaacha kwa muda tofauti zangu za kiitikadi na Godbless Lema na kuungana naye. Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kusapoti kinachofanywa na nabii feki Geor Davie. Yule nabii ana mchango mkubwa sana kwenye umaskini wa watanzania wengi. Mnaosema kwamba Geor Davie ni mtumishi wa Mungu inabidi mpimwe kwanza akili. Ndoa zilizovunjika kisa upotoshaji wa Geor Davie hazina idadi. Wanawake wengi ni wahanga wa utapeli wa huyu nabii feki.

Pia kitendo cha Geor Davie kupanda kwenye jukwaa la siasa la mbunge Gambo linamwingiza moja kwa moja kwenye siasa za Arusha. Angeweza kutoa huo msaada ofisini kwake au hata kufanya tu press conference na sio kwenda kwenye majukwaa ya kisiasa. Kwa msiofahamu ni kwamba hata Gambo mwenyewe ni mbunge ambaye hatakiwi kabisa na wapiga kura wa Arusha. Mwisho wake ni 2025 vinginevyo chama kitapoteza jimbo endapo atasimamishwa kugombea kilazima. Gambo alishawahi tumbuliwa enzi za JK. Hata hayati JPM alitamka hadharani kama kuwa jamaa ni mtu mnafiki na mfitini. Na akamtumbua. Ushirikiano wa GeorDavie na Gambo ni wa hovyo kwa maslahi yao binafsi.

Nakuunga mkono Lema kwenye hii vita dhidi ya nabii feki. Mungu akutangulie maana utaokoa wengi.
Niliachaga kuwasikilizA hao mananbii wa uongo kitambo sana
 
Wewe hujui Kolimba alikufaje?

Ni Sawa na hapo ufipa mnavyosema Nitakuchachawangwe!
Unachanganya hadithi, lakini sishangai, ni sifa ya kijani. Mwisho nikuhamaki lakini ukweli unabaki ukweli. Alitoa mawazo yake juu ya Sera ambazo hazimkomboi Mwananchi!!!!!!!
 
Hudhuria mikutano ya CDM utasikia au fuatilia tang kufunguliwa kwa mikutano! NB; Sheria za Nchi hazimzuii raia kuelezea madhira aliyopitia, mtake msitake kila mmoja ataeleza mateso na maumiv tu haijalishi walinda legacy watachukia ama la!!!
How pathetic! Ushindi hauji kwa hisani! Jengeni hoja acheni kejeli
 
Lema mara zote wanasema ukiwa na hasira sana usiongee lolote .lakini pia ukiwa na furaha jizuie usiongee chochote! Hiyo ndio ilimtokea lema akiwa jukwaani ,kelele za washangiliaji zikamwondolea hekima zikamletea kichaa akajikuta anaanza kulaumu hata watu ambao sio sehemu ya ajenda ya mkutano!! Mfano anamwambia mchungaji na nabii geordavie kwamba alikosea kuwasaidia wananchi badala yake angekarabati kanisa lake ! Hiyo haikuwa na mantiki yoyote kwenye hotuba yake !! Pili anadai biashara ya boda boda ni laana ! Anasahau Ile biashara ni kama biashara zingine !! Anataka kutuambia wanaoagiza pikipiki nje waache kuziagiza kwa kuwa ni laana! Anataka kusema maduka ya pikipiki kariakoo na nchi nzima yafungwe kwa sababu ni laana . Labda alitaka kusema makampuni yapikipiki yaache kuiuzia Tanzania pikipiki kwa kuwa ni laana ?? Watanzania wangapi wanaendesha maisha Yao kwa kutegemea pikipki na bajaji ! Ni Kodi kiasi Gani serikali inapata kwa biashara ya pikipiiki. Lema hotuba Yako imekuondolea heshima mtu mzima huchutama waombe radhi bodaboda nchi nzima maana umewatukana!!!
 
Unachanganya hadithi, lakini sishangai, ni sifa ya kijani. Mwisho nikuhamaki lakini ukweli unabaki ukweli. Alitoa mawazo yake juu ya Sera ambazo hazimkomboi Mwananchi!!!!!!!
Chacha Wangwe alitaka kutumia haki yake ya kikatiba kugombea Uenyekiti!

Kumbe sumu haionjwi!
 
Lema anawaambia ukweli mchungu watanzania.. hadi wale walikuwa wamelala wataamka. CCM sasa hivi wanaona jamaa anawasanulia kuwaamsha maboya wao
 
Katika maelezo yote ni kwamba Lema anaulalamikia Umaskini ulioletwa na CCM lakini anaogopa kuitaja CCM na kujificha kwenye Kichaka cha Magufuli

Ni kweli nchi yetu ina umaskini na Ndio sababu Shujaa Magufuli alipigana hadi mwisho wa uhai wake ili aongoze ukombozi

Lema kaikimbizia familia yake Canada kwa sababu ya Umaskini na Ndio sababu anasema haitarudi

Sasa Chadema itueleze itatukwamuaje katika huu umaskini Bila ya wao Kulamba Asali

Mungu awabariki
What happened. Naona kama vile standard yako imetelemka kwa kiasi kikubwa. Au kuna mtu mwingine huko Lumumba anatumia au mnashare account JF. News ziko below per.
 
Inawezekana unasema kweli lkn huenda wenzetu huko walikuwa wanafanya hizo kazi za ovyo lkn walikuwa na mikakati yakujiondoa walipokuwa na Sasa wamefanikiwa labda uniambie kama ccm inahuo mkakati/mpango wakuvuka hapo

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
Wewe na mimi tulikuwepo awamu ya tano - mikakati tulikuwepo! Ila kwa sasa kusema ukweli sijui! Na wewe Nafikiri hujui! Na ukitaka kwa SAUTI kwamba hujui, utaitwa Sukuma gang! Mimi mikakati wa CCM hii sijaujua.
 
Lema sijui ana elimu ya kiwango gani?, sidhani kama unaweza zungumza hayo ukiwa umefundwa vyema na wazazi wako.
1. huwezi kubeza jitihada za mwingine ktk kutafuta riziki ili naye aishi, bodaboda wanafanya mambo mengi sana hapa nchini, wanalipa kodi, wanasaidia ndugu zao, wanaendesha maisha ya familia zao, wanajiajiri kupunguza vibaka mtaani...wanafanyika baraka kwa watu wengine wanaowazunguka hasa katika kutoa huduma.
2. Nabii huyo hata kama hafanyi kazi kwa kumfurahisha mtu hapa duniani, ila inaonyesha ana upendo kiasi fulani hata kama ni wa kinafki ila anao kwa kuwasaidia wengine, ndio maana hapa duniani hatufanani..mawazo ya lema si mawazo ya nabii, kila mtu afanye lile analolimudu, kama ni kanisa atalijenga na si kwa mapenzi ya lema. 😀 😀
 
Watanzania kuambiwa ukweli mnajitia hasira......Hawa viongozi wa kidini wengi ni msalaba
 
Limbukeni la Canada linachafua chama...
Licha ya Mbowe kuwa tajiri mara kumi au ishirini ya Lema hawezi tukana wananchi masikini namna hii...

Yaani huko Canada kumemfanya atukane kila kitu Tanzania
Halafu atakuja omba Kura Kwa bodaboda
Mimi ni CCM pure. Lakini Mimi nadhan serikali yetu inahitaji kuja na plan kuhusiana na swala Zima la ajira. Ni kweli Toyo imesaidia kupunguza makali ya maisha kwa vijana, lkn zimeleta maafa na ulemavu kwa vijana, maradhi ya pneumonia sugu na ulevi uliopitiliza unaosababishwa na depression. Hao vijana kwa taarifa wanapewa mikataba ya kinyonyaji haswa na wanaowapa hizo PIKIPIKI kwa AHAD za kuzimiliki baada ya muda. Hadi kipindi kifike unakuta PIKIPIKI ni mbovu na ishachakaa.

Zaidi ya hapo nina mashaka na ubora wa vyombo hivyo, hivyo vyombo nchi zilizoendelea haviwezi kuvipokea
 
Ila hizo kazi ni ngumu Sana naona ni kama betting serikali inakusanya kodi nyingi Sana kwa agent anaeingiza pikipiki na agent anapata faida kubwa

Swali la kujiuliza hili ongezeko la pikipiki zimesaidia kwa kiwango gani kupunguza umasikini kuna kundi kubwa la vijana wanakimbilia kwenye hii
Kuna haja ya kufanya utafiti zaidi
 
Nilikuwa sielewi kwanini Magu alitaka kumu wipe huyu fala but now i see. Lema ni bogus tu kama askari wa unguja. 😀😀😀

Unaita kazi inayomlisha mtu na familia yake laana wakati ni kazi halalali. Angekuwa na busara kama angepropose mifumo ya malipo viwandani iwekwe kwa masaa kama ulaya.
Nna imani atarudia maelezo yake. Ujumbe haukufika ilivyotakiwa..
 
Back
Top Bottom