Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Mtu anashinda siku nzima anasajiri lakini bure mwisho wa mwezi analipwa elfu 20. Hizi ni kazi za watu wavivu wasiopenda kazi.

Kwa Mchaga kama Lema huo ni upuuzi.
Kazi za watu wasio wavivu ni zipi ? Na zipo wapi hapa Tanzania ?
 
Namsikiliza mbunge wa zamani ndg Lema Jembe fm, anahojiwa alipokeaje suala la yeye kufutiwa kesi zake.

Lema anadai moja ya vitu anavyompongeza mama ni pamoja na yeye kufutiwa mashtaka pia mikutano ya kisiasa...
Yuko sahihi, ni vizuri kuwa mkweli kuliko kuwa mwanasiasa mnafiki
 
Godbless Lema ni mwanasiasa contraversial na anaependwa sana Jijini Arusha. Kinachompa umaarufu sasa ni kurejea nchini kutoka Canada, ni kama vile bado ana kimuhe muhe cha kutaka kuelezea alichokiona Canada kulinganisha na nyumbani Tanzania.

Ameanza kwa kukosoa kazi za boda boda, vikundi vya Vicoba, na mengine. Swali la kujiuliza ni kwamba, yeye mwenyewe anafanya biashara gani inayomlipa?

Hawa vijana wataenda wapi? Ndio sio sawa ila lazima wapate makazi, chakula na kulea watoto wao vizuri. Je, tuna lolote la kujifunza kutoka kwa Godbless?

What businessess are you in Sir?
 
Namsikiliza Mbunge wa zamani Nndg Lema Jembe FM, anahojiwa alipokeaje suala la yeye kufutiwa kesi zake.

Lema anadai moja ya vitu anavyompongeza Mama ni pamoja na yeye kufutiwa mashtaka pia mikutano ya kisiasa...
Watu ambao watoto wao huwa bado ni vitoto havijui utamu wala uchungu wa maisha , kwa kawaida huwa waropokaji sana wanapowaangalia vijana wa watu wengine wanavyoteseka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…