King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Tatizo binadamu hawapendi kuambiwa ukweli,Ipo hivi unaweza ukadhani anaongea masihara lakini ndiyo ukweli HALISI .. kuna kazi unafanya kwenye mazingira magumu jua kaliiii lakini hata ufanye mpaka Kufa huwezi kuaga umaskini., Zaidi ya hapo utapata pesa ya kula tu na kijikimu masuala mengine kama mavazi.
So kwa upande wangu Lema yupo sahihi, Serikali ijaribu kutengeneza fursa ambazo watu wakifanya wataweza kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi.... Mfano kilimo Bora, Uvuvi bora ambao unahusisha teknolojia na wahamasishe Vijana kuingia kwenye sekta ambazo zinaweza kumtoa mtu hatua moja kwenda nyingine,na sio kuchekea vijana nguvu kazi kutembea juani na mabegi ya ukwaju.
Na kuliko kufanya kazi kama kusajili laini kazi ambayo naamini wahusika wanalipwa Commission ndogo, huku laini wanazosajili zikienda kuwaingizia makampuni ya mitandao ya simu mabilioni ya pesa...
Tuna njia ndefu kama Taifa kupiga vita umaskini.
Mkuu nikuulize leo hii una kijana wako ungependa asajili line kama kazi ya kumuingizia kipato?territorial captivity release and freedom inamsumbua sana Lema
Wakati ccm inafanya kitu hao vijana wafanyeje?Ameiambia ccm ifanye kitu msianze kumshambulia.
Tatizo la maskini akiambiwa ukweli anachukia badala ya kutafakari
Hamna ambaye hataki kijana wake apigwe kiyoyozi na kulipwa atleast million 5 kwa mwezi. Shida hizo kazi za maslahi hayo zina wenyewe.Mkuu nikuulize leo hii una kijana wako ungependa asajili line kama kazi ya kumuingizia kipato?
Lema ni mpuuzi sana japo chadema watakuja apa kumtetea anaongea vitu apate fame na attention Kwa sababu ameona watz ni watu wa ku entertain vitu vya kijingaUnaposema boda boda ni kazi ya laana, kusajili laini ni kazi ya kipuuzi hutaki mwanao umuone anaifanya utamfukuza kwako, vikoba ni laana sijui hutaki mkeo ajihusishe navyo kabisa...
Huoni cost zitakua juu, na ku compensate kampuni zitaongeza bei ya huduma kufidia?,Wafanyakazi wa kampuni za simu, wale wanaokaa kwenye kiyoyozi kwenye maduka.
Mdogo wangu aliajiliwa makampuni ya solar akawa anazurula kutwa nzima mwisho wa mwezi anapewa elf 30 nikamwambia acha hio kazi au nikufukuze kwangu aka anza kufuga kuku sasa hivi yupo vizuri ana duka la mtaani mwanga anauona
It can be a stepping stone while figuring something else, sometimes I may use that one to assess her attitude towards self reliance.Mkuu nikuulize leo hii una kijana wako ungependa asajili line kama kazi ya kumuingizia kipato?
Kaka wewe na Lema toeni solution, stop the complains and blame game. Hamna ambaye haelewi kuwa bodaboda sio career.Lema yupo sahihi watu tunampinga bite tu na ndio maana takwimu ya watu wasio nafuraha duniani tz huwa hatukosi kwa sababu hizi hizi kuwa na. Kundi kubwa la ajira za u ababishaji ambapo kipato chake ni Bora kula so chakula Bora
Akimfukuza ndio anakuwa amemsaidia nini?"Nikisikia mwanangu ni bodaboda au anasajili laini inabidi atafute sehemu ya kukaa, kwangu simtaki tena," alisema Lema.
Hapo hamna haja ya uchunguzi, fuse ya unyolo ilishakatwaTumchunguze vizuri huyu jamaa kipindi kile amevaa baibui huenda....
π¬π¬kazi ya saa 1. Huku unapigishwa mzigo masaa 12 unalipwa elfu 4 na hamna kitu utaongea.
Faamasiala nini πππ sasa utachagua ukabebe makreti kwa Mo au uendeshe boda boda kwa masaa hayo hayo upate elfu 30.π¬π¬
Hata udreva wa mabasi ni kazi ya hatari sana,, lakini haina maana mabasi yapigwe marufuku, watu kwa maelfu wanakufa kwa mwaka kwa ajali za mabasiLazima kama Nchi tuhakikishe vijana wanapata ajira za viwandani au mashambani , kule Kyela siku za nyuma kidogo kulikuwa na vijana waliokuwa wakifanya biashara ya kusafirisha mizigo mizito kwa baiskeli , walijulikana kwa jina la NJEMUKE ( kwa kiswahili ni kama kuchemka au kutobweteka )
Hawa walitumia baiskeli ya Phoenex , sijui ilitengenezwa wapi , walibeba mizigo mizito sana huku wakiendesha baiskeli hizi , lakini baadaye wakaanza kupukutika kwa maradhi ya kifua hadi tukaaanza kuwapa elimu kwamba ni bora waingie kwenye kilimo .
Kwahiyo watu waweza kuwa wanafanya jambo linaloonekana linawasaidia lakini kumbe nyuma yake kuna madhara makubwa