Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

CCM wawe makini na kauli hizo za lema, kwenye mikutano yao ya hadhara wanamjibu kwa kujipendekeza kwenye makundi hayo wakati inaonekana wazi bodaboda na VICOBA ni ishara ya wazi kabisa kuwepo kwa umasikini na ufukara katika jamii
 
Maisha yetu magumu sana lakini hamna mzazi anayelipa ada ili mwanae aje kuwa bodaboda.

Hamna mzazi anayepata mimba na kuwish atakaye mzaa aje kusajili line
Wishing and getting are different. Unaweza kuwish lakini uhalisia ukawa mwingine
Lema hana substance. Anaeleza end result ya tatizo bila kuleta suluhisho la tatizo lenyewe.
Alikuwa mbunge wa Arusha mjini kwa miaka 10. Kulikuwa hamna bodaboda?Kulikuwa hamna wasajili line, wamama wauza nyanya ?

Alifanya nini kuondoa hali hiyo?Jiji la Arusha wakati huo lilikuwa chini ya Chadema alitoa mchango gani? Madiwani wote walikuwa Chadema isipokuwa kata moja ya kati Arusha mjini. Lema amekuwa populist wa kupiga kelele. Malkia mmoja wa Ufaransa kabla ya mapinduzi ya Ufaransa alisimama kwenye balcony na kushangaa watu wanaandamana kupinga uhaba wa mikate.Akasema kama kuna uhaba wa mikate kwanini wasile keki.

Lema amekuwa mjinga baada ya kupata exposure. Nilidhani kukaa Canada kutamuongezea uwezo wa kutafakari. Anashauri watu wasiokuwa na means zingine wafanye nini?
 
Mwache Lema atupe hiyo 'exposure' ya kuishi CANADA kwa mwaka mmoja na atufundishe jinsi maisha yanavyopaswa kuwa hata kama ni kwa kutusimanga.Kuna wengine wameishi huko miaka zaidi ya 20 lakini hawajapata 'exposure' kama ya Mh.Lema. What a genius man,mwaka mmoja tu amerudi ni mwalimu wa kila kitu [emoji3]
 
Jamaa ni kama yule kipofu alieona punda

Kufika Canada ameona kama miujiza ameshangaa na ni ushamba tu kuona maisha ya huko ni tofauti

Angekaa miaka 10 angetukana wanaokula Ugali Walahi
Nawajua baadhi ya watu wanapokuja nje na wwkirudi nyumbani hujiona wamebadili maisha na kuwaona wengine kama mbuzi tu

Nimekaa nje karibia miaka 50 ila hata siku moja sijawashangaa maisha ya jamaa zetu huko ila nawaombea always maisha yawabadilikie

Anawatukana watu wakati yeye na familia wanakula hela za wakimbizi
Amejilipua ukimbizi na kujidhalilisha kwa wazungu
Watoto wanasoma kwa jasho la walipa kodi Canada

Badala aseme njia mbadala yeye anayashangaa maisha aliokulia mpaka kafika hapo

Anafananisha Canada na Tanzania anataka wawe sawa

Jamaa kumbe ni mshamba kiasi hicho
Ulimbukeni mbaya sana
Kufika Canada kaanza kutukana washikaji
Mzabeni makofi huyo [emoji1]
 
Bodaboda wengi wanakubaliana naye. Wanakubali kuwa kazi yao ni ya laana kwa namna wanavyochukuliwa, pia kwa mambo wayafanyayo kupitia hiyo kaxi.
Zaidi hata wao kuna wanasema wanaiganya kwa kuwa hawaona namna nyingine na kuna wanaoifanya lakini wanapambana zaidi ili waachane nayo.

Ushauri wangu. Watafuteni hao bodaboda ili mbadilishane kazi, wapeni zenu, mchukue za kwao
 
Lema amekuwa mjinga baada ya kupata exposure. Nilidhani kukaa Canada kutamuongezea uwezo wa kutafakari.Anashauri watu wasiokuwa na means zingine wafanye nini?

Tatizo anajiona yeye ndiyo amekuwa mtu wa kwanza Mtanzania kwenda kuishi Canada tena kwa mwaka mmoja tu.Zamani nilikuwa namsikiliza lakini kwa sasa namuona kama limbukeni flani tu.Usije kuta kwa sasa hata chakula atawaambia wampikie kama alichokuwa anakula Canada.
 
Unahitaji akili gani kufanya kazi ya bodaboda au kusajili laini??
Hiyo inayomfanya ajue wapi ni wapi
Kwani hao wenye PhD wamesaidia nini katika kukuza ajira zaidi ya akili za mikopo?

Vijana wanahitaji muwasaidie kama hamtaki wafanye hizo kazi
Sawa haihitaji taaluma kubwa ila suluhu ni ipi?
 
Huo ndio ushauri wangu kwa ndugu Lema. Naamini hamna mtu atakataa kazi ya kuwa Kamishna wa TRA au Naibu waziri
 
Afadhari nyie mliokaa nnje kwa muda mrefu msaidieni apunguze ujuaji wa kuishi Canada kwa muda mfupi.Anakoelekea anageuka kuwa kichekesho
 
Inawezekana Lema ameshindwa kukielezea anachowaza kwa ufasaha.

Bodaboda ni ajira kwasababu vijana hawana namna lakini kwa Taifa masikini binafsi naamini ni upotevu wa nguvu kazi na wakulaumiwa sio Bodaboda bali ni watawala kushindwa kuwa na mipango mizuri na sahihi kwa vijana.

Tunapaswa kuilamu Serikali kwa kushindwa kutanua uwanja na kuifanya jamii kuwa na fursa nyingi zenye vipato na kuboresha maisha ya wati kuliko hivi sasa.
 
Leo mmemgeukia JPM na sera ya viwanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nisaidie kumuuliza hii boda yangu nauza nipige mishe gani isiyo ya laama kwa uwezo wangu?
 
Wakuu huyu bwana anayeongea kama amekatwa kichwa Arusha imejaa wauza mitumba kila kona toka ubunge wako mpaka sasa lakini haukusema ni kazi ya laana wala kuonyesha juhudi za kuwasaidia vijana wa Arusha
 

Huyo muache alivyo. Anadanganya umma mchana kweupe bila ya soni. Eti anasema Canada 90% ya wananchi wake wanamiliki nyumba. Hivi anajua kweli gharama ya kumili nyumba kwa nchi za ulaya na marekaniii.
 
Lema anaweza kuwa na hoja, tatizo ni uwasilishaji wa hoja zake, anavyoongea namuona kama mtu anayejifikiria mwenyewe, anatakiwa aseme sasa badala ya kusajili line wafanye kazi gani nyingine ili wajikimu kimaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…