Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Maisha yetu magumu sana lakini hamna mzazi anayelipa ada ili mwanae aje kuwa bodaboda.

Hamna mzazi anayepata mimba na kuwish atakaye mzaa aje kusajili line
Mrembo, kusajiri line ni kazi ambayo hata huko Canada na marekani wanafanya, tofauti tu ni kwamba kwao malipo ni mazuri kupita kwetu. Makampuni yote ya simu yana ofisi ambapo wateja wapya husajiri line na kulipia bill zao. Na kuna kampuni binafsi hufanya kazi hizo kama independent agents wa kampuni za simu. Asikudanganye mtu dada yangu.
Hata hiyo Bodaboda, kwao sasa hivi kuna Ubber na Lyft, tofauti yake na bodaboda wetu ni kuwa wao wanatumia magari sisi tunatumia pikipiki, kazi ni ile ile!
Lema anasumbuliwa na mambo makubwa mawili:
1. Ulimbukeni. Amefika Canada kwa hiyo anaona dunia yote lazima iishi kama Canada! Amesahau hali halisi ya kwao huko uchagani alikotoka.
2. Lack of education and intelligence. Kwa mtu mwenye akili timamu ya kuelewa mambo angekumbuka kuwa huko aliko anapewa kila kitu (nyumba, chakula, shule za watoto, utilities, nk) bure na serikali ya Canada kwa sababu ya status yake ya ukimbizi. Ebu awaulize waliokwenda huko kwa mishe zao bila kubebwa aone kama watasema kupiga box ni kazi ya kimaskini. Mtu anayepewa kila kitu bure na mtu anayejitafutia mwenyewe ni watu wawili tofauti kabisa.
 
Ni muendeleolzo wa muinjilisti Lema na Mwanasiasa anaeongea ukweli siku zote.

Zikiwa ni siku kadhaa tangia amerudi mafichoni Canada na kuja kumkalia kooni Nabii wa Mchongo Deodavie ya kuwa ni mpuuzi mmoja anaeaminiwa na watu walikosa maarifa.

Lema anasema kuwa maisha ni magumu halafu Nabii anatangaza kuwa kutakuwa na maombi ya kufungua vifungo na baraka kwahiyo tumeni michango yenu elfu 20. Wakati hiyo elfu 20 mwananchi alitakiwa kwenda kununua unga na mchele ukale na familia yako, lakini watu wanaenda kutoa kwa Nabii Deodavie.

Lema endeleaa kuwapiga spana hawa watu.
 
Lema anajidai kuwasanifu madereva wa bodaboda na kutamba kwamba yeye yuko vizuri. Kwanza ni mjinga anashindwa kutambua hakuna kazi halali isiyokua na madhara ya muda mrefu kiafya. Pia atambue kupanda kimaisha ni jukumu la mtu binafsi. Ukiwa dereva wa bodaboda uwe na mpango wa kupanda kimaisha kwa nini usifanikiwe.

Inadaiwa lema alikua mwizi wa magari. Hiyo kazi kama alifanya au hakufanya ni uzushi tu bila shaka ilikua hatari kuliko kuendesha bodaboda. Lakini alitokaje hapo kama ni kweli mwenyewe ndio anajua.

Kwa hivyo yafaa aache kudharau wengine na kujidai. Yeye alifeki ukimbizi na tunashukuru zito katoa hii siri. Amelipwa kwa ukimbizi feki huko canada na sasa ametumwa kuwachanganya watu.

Yote anazungumza wala hayafai kwa mpango wetu kwa maendeleo. Mara uraia pacha mara bodaboda hazifai ni hatari wakati mwenyewe kaanza na kazi hatari sana.

Yaani anazungumza mambo ya vijiwe ili kupata sapoti ila kwa uhakika hajafanikiwa. Bado tu hajatetea ushoga🤣
 
Lema anajidai kuwasanifu madereva wa bodaboda na kutamba kwamba yeye yuko vizuri. Kwanza ni mjinga anashindwa kutambua hakuna kazi halali isiyokua na madhara ya muda mrefu kiafya...
Hapo umemshambulia tu. Na yawezekana ni wivu. Ungeeleza hizo hatua na uelezee kuhusu ubora na usalama wa kazi ya bodaboda.
 
Baada ya Yesu kutamka maneno haya " Naona Kiu" hekaheka zikawa nyingi sana pale chini ya msalaba kila mtu akija na tafsiri yake

Nimemuelewa Nabii Godbless Lema japo kisiasa Siyo rahisi kukubaliana naye

Wanasiasa Wengi hawana Kiu bali Wana Njaa ndio sababu ni rahisi kwao kuukumbatia Uovu badala ya ile Kweli

Mungu humtumia yoyote kufikisha Ujumbe wake kwa wanadamu

Je, ni Kweli Lema hana njaa ana Kiu ya Ukombozi?

Muda utasema!
 
Umeniwahi mkuu! Sabaya anajua Kwan yupo pale! Spika aiyepita anajua Lema ananini

Lema ni mtu wa fact
 
Hapo umemshambulia tu.Na yawezekana ni wivu.Ungeeleza hizo hatua na uelezee kuhusu ubora na usalama wa kazi ya bodaboda.
Nimuonee wivu mkimbizi feki? Kwani anavyojidai ana biashara canada unafikiri ndio kashafanikiwa? Labda kwa kulipwa kwa kukubali ukimbizi feki. Canada sio mbinguni watu tunafahamu fursa gani zipo.
 
Polisi waliziita ndoto za Nabii Lema kuwa ni uchochezi, ama? Lakini kwa tunaomtii Mungu kila ndimi linalotaja Mungu ikiwa ni muovu tutalitii jina la Mungu pasipo kujali limeletwa kupitia mtu wa aina gani
 
Nimuonee wivu mkimbizi feki? Kwani anavyojidai ana biashara canada unafikiri ndio kashafanikiwa? Labda kwa kulipwa kwa kukubali ukimbizi feki. Canada sio mbinguni watu tunafahamu fursa gani zipo.
Ndiyo uwaoneshe bodaboda hizo fursa unazozifahamu ili Lema aache kelele.
 
Mkuu sio kweli
 
Naona Lema kaamua kuwananga wapiga kura wa CCM...
 
Nabii si angefungua kanisa kama yeye ni nabii. Analeta swaga za Mwalimu aliekuwa anaangalia TV ikulu na kuja kusema ameota.
Utakuwa wa makamo mwenzangu umenikumbusha stori za Mchonga..any ways hata kwenye biblia Kuna manabii wengi hawakuwa na masinagogi🏃🏃
 
Toka ametoka nje sijamuelewa maneno yake anaongea vitu ambavyo kisiasa siyo muhimu wala lazima kuvisema, kiufupi havina tija wala maslahi yoyote kwa chama chake.

Inawezekana ni ugeni wa kukaa nje au pride ya Kichaga imekolea, ila ni hatari kwa usalama wa chama kisiasa, kwa sababu watu anaowahutubia wengi hawana upeo mkubwa wa kuchambua mambo kama yeye.

Nashauri CHADEMA tafuteni namna ya kumshauri aachane na hayo mambo ya kushambulia makundi muhimu, mpunguze taharuki. Kipindi hiki hamuhitaji kuwachanganya watu. Kila mtu ni muhimu.

Siasa ni sayansi, siasa pia ni hesabu. Inabidi kuwa makini sana na maneno, na pia namna ya kuzungumza hayo maneno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…