Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Ni sawa, ila LEMA naye anapaswa kuchuja vitu anavyoongea na apunguze jazba.

Anapaswa kujua uelewa wa Watanzania wengi ukoje hasa jamii ya watu hao kama bodaboda na wanawake wajasiriamali wa sokoni na magengeni.

Yeye badala ya kuongelea HOJA za msingi na kueleza kipi ataweza kufanya kwa wananchi kupitia chama chake yeye anaongea hovyo, nathubutu kusema ANAROPOKA.

Alishaongea pia hovyo pale sokoni Samunge.
 
Habari!
Wao boda wameacha maneno yote ya Lema wamechukua neno laana tu na kuanza kutembea nalo.
Na CCM wameshapata mpenyo chap wameingilia kati.
Ni kweli hata China , India n k kuna bodaboda lakini hilo lisitumike kuhalalisha hii kazi hatari inayozalisha walemavu kila siku nchini.
Hilo pia lisitumike kuhalalisha kazi ya bodaboda ambayo imesababisha watoto kukosa baba kila siku kutokana na ajali za bodaboda.
Vipi tumewahi kufikiri uzeeni hawa bodaboda wataenda wapi, wataishi vipi?.
Siasa za Tanzania ni za kuviziana. Bodaboda walipaswa kuungana na Lema kudai ustawi wao lakini wamekaa kimya, CCM wameingia na kujifanya wapo pamoja na Bodaboda mpaka mwisho wa safari ilhali watoto wao wanawapa ajira Usalama wa Taifa na ubalozini.
Ile siku ommy anaondoka pekeake ndipo alipata ajar pale uhasibu juu darajani ilikua one way enzi izo....

Nipale watu wanapo amua kuelewa wanacho kielewa... upotoshaji umetamalaki...

Mpk Leo ommy mguu wake mmoja ni mfupi for sure bila pesa pale MOI wangemkata mguu .....
 
Habari,

Wao boda wameacha maneno yote ya Lema wamechukua neno laana tu na kuanza kutembea nalo.

Na CCM wameshapata mpenyo chap wameingilia kati. Ni kweli hata China, India n.k kuna bodaboda lakini hilo lisitumike kuhalalisha hii kazi hatari inayozalisha walemavu kila siku nchini.

Hilo pia lisitumike kuhalalisha kazi ya bodaboda ambayo imesababisha watoto kukosa baba kila siku kutokana na ajali za bodaboda.

Hivi tumewahi kufikiri uzeeni hawa bodaboda wataenda wapi, wataishi vipi?

Siasa za Tanzania ni za kuviziana. Bodaboda walipaswa kuungana na Lema kudai ustawi wao lakini wamekaa kimya, CCM wameingia na kujifanya wapo pamoja na Bodaboda mpaka mwisho wa safari ilhali watoto wao wanawapa ajira Usalama wa Taifa na ubalozini.
Bodaboda wameathirika the so called Stockholm Syndrome. Msiwashangae bali muwahurumie
 
..ukimsikiliza lissu..msomi.aliyekaa nje mda mrefu kuliko lema (asiyesoma) utaona tofauti ya hoja zao sana ..lema yuko nje sana ya uhalisia kwenye hoja zake..wakati lissu anajenga hoja kwa kuendana na uhalisia...
 
Ngoja nijibu kama hivi;

1/ Amesema ni kazi ya Laana pengine sababu namna wanavyotumiwa na Wanasiasa kwenge ajenda zao,ila kiukweli ni kazi kama kazi zingine,watu huendesha maisha yao kwa hiyo kazi.

2/Tatizo la ajali za Boda boda,asilimia kubwa ni uzembe wao binafsi, wengi hawafuati sheria za barabarani haswa speed na hili linatokana na namna hawa wanavopata leseni zao,mafunzo ni mtaani mtaani tu.

3/Wengi hii kazi wameingia kama tegemeo la mwisho, baada ya ajira kuwa shida, hii taswira inaweza badilishwa kwa kuwekewa mifumo rasmi,itambulike kama ajira zingine.

4/Kuna hoja ya uzeeni wataishije, hii itufungue namna ya kuwasaidia kuwapa elimu namna ya ku save for the future.

5/Serikali iangalie namna ya Kukuza sekta ya kilimo,naona huku tunaweza jificha vijans wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaposema boda boda ni kazi ya laana, kusajili laini ni kazi ya kipuuzi hutaki mwanao umuone anaifanya utamfukuza kwako, vikoba ni laana sijui hutaki mkeo ajihusishe navyo kabisa.

From a standing point wewe ni mkimbizi wa kisiasa umebebwa huko Canada for over a year. Umepata PR na familia yako na privileges nyingi huko. Umeyaona maisha kwa utofauti hilo hatukatai. Najua kwa sasa wewe watoto wako wanaweza wakaishi huko Canada for whatever reasons, huko ada hazilipwi ni serikali kila kitu. Mzazi kazi yako ni kulipa kodi ya nyumba na utilities tu.

Viwanda na Private companies ziko kibao kiasi kwamba ishu ya kupata cha kufanya wakimaliza vyuo ni wao kuamua tu kukaa kwenye corporate sphere, kwenda kuuza migahawa, kukwangua mabarafu na kutawaza wazee.Maybe sio kazi za hovyo atleast kwa uchumi wa Canada maana hata wazungu wenyewe wa huko hawazitaki.

That being said, wewe unapata wapi guts za kusema kuwa Watanzania wanafanya kazi za laana esp. Boda boda, wasajili line na wauza mboga wanaocheza vikoba? Okay, hizo kazi ni za laana atleast kwa fikra zako lakini ushajiuliza kuna ugumu kiasi gani kwa hapa Tanzania when it comes to making ends meet?

Sidhani kama una idea kwamba graduate aliyemaliza chuo anaetoka familia hohehae anapitia ugumu kiasi gani na fedhea ilioje pale anapokosa ajira na hana mtaji! Usicheze na maisha ya watu kabisa, huna ajira una mke na mtoto huna chanzo cha pesa unafikiria kitakachofuata nini?

Utakaa chini unaangalia familia iangamie? Boda boda ndio quick fix ya maisha yetu ya dhiki walau familia zile na maisha yaende, vikoba ndio quick fix ya mikopo ya benki bila masharti magumu.

Toa solution watu wafanye nini baada ya kuachana na hizo kazi za laana. Sio unaropoka hovyo tu bila kuwa na substance. Tanzania sio Canada watu wanakolipwa dollar 15-20 kwa kazi ya saa 1. Huku unapigishwa mzigo masaa 12 unalipwa elfu 4 na hamna kitu utaongea.
Kwa Kweli Hadi mkuu extrovert umeandika Uzi bas Ni kwamba umekereka Kam mm kwa kauli za huyo mpuuzi wa chadema kuita Kaz. Ni laana ni mikosi anajitafutia kenge huyo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Fikiri kabla ya kutenda, ila watu maarufu wengi huwa hawawazi nini cha kuongea mbele ya kamera, na kwenye kadamnasi
 
Habari,

Wao boda wameacha maneno yote ya Lema wamechukua neno laana tu na kuanza kutembea nalo.

Na CCM wameshapata mpenyo chap wameingilia kati. Ni kweli hata China, India n.k kuna bodaboda lakini hilo lisitumike kuhalalisha hii kazi hatari inayozalisha walemavu kila siku nchini.

Hilo pia lisitumike kuhalalisha kazi ya bodaboda ambayo imesababisha watoto kukosa baba kila siku kutokana na ajali za bodaboda.

Hivi tumewahi kufikiri uzeeni hawa bodaboda wataenda wapi, wataishi vipi?

Siasa za Tanzania ni za kuviziana. Bodaboda walipaswa kuungana na Lema kudai ustawi wao lakini wamekaa kimya, CCM wameingia na kujifanya wapo pamoja na Bodaboda mpaka mwisho wa safari ilhali watoto wao wanawapa ajira Usalama wa Taifa na ubalozini.
Wanasiasa hutumia ujinga wa wananchi kupitia kura
 
Sio Lema tu Chadema imeejaa wapuuzi wengi sana ambao wamekuwa entertained kwa miaka mingi sana.

Wameharibu akili za vijana wengi mno.
Yaani hapa umanena ,chadema wameharibu vijana hadi wasomi walioamua kabisa kuwa wajinga kama ambavyo Diamond kaweza kupata wafuasi kwa nyimbo za matusi tu
 
Jamaa ni kama yule kipofu alieona punda

Kufika Canada ameona kama miujiza ameshangaa na ni ushamba tu kuona maisha ya huko ni tofauti

Angekaa miaka 10 angetukana wanaokula Ugali Walahi
Nawajua baadhi ya watu wanapokuja nje na wwkirudi nyumbani hujiona wamebadili maisha na kuwaona wengine kama mbuzi tu

Nimekaa nje karibia miaka 50 ila hata siku moja sijawashangaa maisha ya jamaa zetu huko ila nawaombea always maisha yawabadilikie

Anawatukana watu wakati yeye na familia wanakula hela za wakimbizi
Amejilipua ukimbizi na kujidhalilisha kwa wazungu
Watoto wanasoma kwa jasho la walipa kodi Canada

Badala aseme njia mbadala yeye anayashangaa maisha aliokulia mpaka kafika hapo

Anafananisha Canada na Tanzania anataka wawe sawa

Jamaa kumbe ni mshamba kiasi hicho
Ulimbukeni mbaya sana
Kufika Canada kaanza kutukana washikaji
Mzabeni makofi huyo [emoji1]
Ukisikia mjinga aisee huyu jamaa amepitiliza
 
Back
Top Bottom