Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Lema ni nabii alisema bwana yule aache Mambo ya ovyo au ataenda zake ikawa. Sasa swala la bodaboda mmemulewa vibaya ..dongo kaipiga serikali kuona bodaboda ni ajira..watu wanalala maofisini Hawana vision kwa Taifa hili ..tuna maliasili kibao kwenye nchi lakini tumezikalia tu...A blessing in disguise
Nabii si angefungua kanisa kama yeye ni nabii. Analeta swaga za Mwalimu aliekuwa anaangalia TV ikulu na kuja kusema ameota.
 
Hapo kwa Boda Boda na mama lishe naomba uzingatie Speed governor.
Katika hilo kundi kuna literate na illiterates.

The forementioned wana extra options sababu wako na academic certificates ambazo ni kama silaha kwa nchi yetu hii wanaajirika when neccessary.

The later wao hawana option zaidi ya kugaragara kwenye uchuuzi tu na boda boda. Watabadilisha kazi ila ni humo humo labda wahamie kwenye kuchoma kuku barabarani.

I Agree with you kuwa Lema ni duanzi na serikali lazma ifanye majukumu yake.
☑️
 
Nchi ya ajabu sana hii. Mtu aliyekua mwizi wa magari na mwenye elimu ndogo anapokelewa na watu wengi hadi anapoteza ufahamu na kuonesha ujinga wake wote.
 
Wanasaidia sana japo ni very risky, jana usiku ilikuwa nimuue moja na abiria wake Morogoro road. Anakuja site ambayo gari zinaenda namie ndio nimechomoa gari naikata Eiecher ile narudisha upande wangu tu huyu hapa nikapiga brake ghafla ndio pona yake. 🤣🤣🤣
Kwani unaendesha gari gani mkuu??
Nimawazo yake huwezi kaumu japo alitumia neno kakasi... kiukweli bodaboda nikazi ya hovyo (ajali mkononi). Vijana wajae kwenye kilimo,kufuga na ufundi siyo kwenye bodaboda nihatari sn kwaustawi wa taifa. Bora ziwe nyingi bajaji sio boda
 
Kimsingi hujapinga hoja za Lema bali unamlaumu kwa kuongea kwake kwa sauti kubwa
 
Ndio madhara ya kwenda abroad kuishi haya,ukirudi kila mtu unamwona mshamba,kapitwa na wakati,ananuka,hana elimu wala hana future[emoji28][emoji28].

Kama ana watu wa karibu aambiwe apunguze speed barabara sio ndefu mbele na haijanyooka sana.
Kwani Lema ndio mtu wa kwanza kuishi abroad? Hivi ameishi muda gani?
 
Kwani unaendesha gari gani mkuu??
Nimawazo yake huwezi kaumu japo alitumia neno kakasi... kiukweli bodaboda nikazi ya hovyo (ajali mkononi). Vijana wajae kwenye kilimo,kufuga na ufundi siyo kwenye bodaboda nihatari sn kwaustawi wa taifa. Bora ziwe nyingi bajaji sio boda
Toyota Surf
 
Unaposema boda boda ni kazi ya laana, kusajili laini ni kazi ya kipuuzi hutaki mwanao umuone anaifanya utamfukuza kwako, vikoba ni laana sijui hutaki mkeo ajihusishe navyo kabisa.

From a standing point wewe ni mkimbizi wa kisiasa umebebwa huko Canada for over a year. Umepata PR na familia yako na privileges nyingi huko. Umeyaona maisha kwa utofauti hilo hatukatai. Najua kwa sasa wewe watoto wako wanaweza wakaishi huko Canada for whatever reasons, huko ada hazilipwi ni serikali kila kitu. Mzazi kazi yako ni kulipa kodi ya nyumba na utilities tu.

Viwanda na Private companies ziko kibao kiasi kwamba ishu ya kupata cha kufanya wakimaliza vyuo ni wao kuamua tu kukaa kwenye corporate sphere, kwenda kuuza migahawa, kukwangua mabarafu na kutawaza wazee.Maybe sio kazi za hovyo atleast kwa uchumi wa Canada maana hata wazungu wenyewe wa huko hawazitaki.

That being said, wewe unapata wapi guts za kusema kuwa Watanzania wanafanya kazi za laana esp. Boda boda, wasajili line na wauza mboga wanaocheza vikoba? Okay, hizo kazi ni za laana atleast kwa fikra zako lakini ushajiuliza kuna ugumu kiasi gani kwa hapa Tanzania when it comes to making ends meet?

Sidhani kama una idea kwamba graduate aliyemaliza chuo anaetoka familia hohehae anapitia ugumu kiasi gani na fedhea ilioje pale anapokosa ajira na hana mtaji! Usicheze na maisha ya watu kabisa, huna ajira una mke na mtoto huna chanzo cha pesa unafikiria kitakachofuata nini?

Utakaa chini unaangalia familia iangamie? Boda boda ndio quick fix ya maisha yetu ya dhiki walau familia zile na maisha yaende, vikoba ndio quick fix ya mikopo ya benki bila masharti magumu.

Toa solution watu wafanye nini baada ya kuachana na hizo kazi za laana. Sio unaropoka hovyo tu bila kuwa na substance. Tanzania sio Canada watu wanakolipwa dollar 15-20 kwa kazi ya saa 1. Huku unapigishwa mzigo masaa 12 unalipwa elfu 4 na hamna kitu utaongea.
Kumbe mara Moja Moja ukitibiwa mirembe Huwa una point 🤪🤪

Lema ni taahira ,kuosha nepi za wazee wa Canada basi anajikuta mjanja saaana
 
Usipokuwa makini kwenye hoja za Lema unaweza kuishia kumtukana, kumkeheli n.k

Lakini mtoa hoja nawe umekosa hoja. Umesema huko Canada kuna kazi za kuosha vyombo, wazee na kusafisha barafu etc ambao hata wenyeji hawazitaki. Unajua maana yake "hao ndio bodaboda, wasajiki line wa huko". Lakini serikali yao itasema kuna watu wamepata ajira kwenye hizo kazi.

Hoja ya msingi ni kwamba wananchi wanataka kazi bora zenye usalama wa maisha yao ya sasa na baadae, zenye kipato cha uhakika, zenye kutambulika rasmi kwenye soko la ajira, na sio kazi za shuruba na malipo yasiyokizi hadhi.

Mfano: wasajili line hawana mshahara bali wana commission ambayo wengi hawafiki 150,000 hata NSSF, hana bina ya afya, hayupo kwenye WCF. Hivyo akiugua, akiumia au kupata janga lolote ajira yake haimsaidii chochote.

Je hiyo ni ahira kweli?

Je akifikisha 45yrs anaweza kuifanya tena anakuwa amestaafu bila malipo.

Je maradhi apatayo kwa kuendesha boda ambayo mengi hijitokeza ukubwani ataweza kuyamudu.

Tuwagafutie watanzania ajira bora hizi za line na boda sio ajira bali laana, mengi tutayaona muda si mrefu.
 
inawezekana anatamani kuyafuta aliyotamka lakini amechelewa kwakuwa huenda aliongea kwa mihemko
 
"Sidhani kama lema ni mzima wa afya ya akili, tumuombee kwa Mungu amponye kwa tatizo alilonalo "
 
Habari,

Wao boda wameacha maneno yote ya Lema wamechukua neno laana tu na kuanza kutembea nalo.

Na CCM wameshapata mpenyo chap wameingilia kati. Ni kweli hata China, India n.k kuna bodaboda lakini hilo lisitumike kuhalalisha hii kazi hatari inayozalisha walemavu kila siku nchini.

Hilo pia lisitumike kuhalalisha kazi ya bodaboda ambayo imesababisha watoto kukosa baba kila siku kutokana na ajali za bodaboda.

Hivi tumewahi kufikiri uzeeni hawa bodaboda wataenda wapi, wataishi vipi?

Siasa za Tanzania ni za kuviziana. Bodaboda walipaswa kuungana na Lema kudai ustawi wao lakini wamekaa kimya, CCM wameingia na kujifanya wapo pamoja na Bodaboda mpaka mwisho wa safari ilhali watoto wao wanawapa ajira Usalama wa Taifa na ubalozini.
 
Ni kweli hata mimi nimejaribu kusikiliza speech yote ya Lema nikagundua aliongea ukweli na lengo lake ilikuwa kuwatetea vijana kuandaliwa mazingira ya ajira rasmi.

Alifafanua vizuri tu jinsi Bodaboda zinavyoongoza kwa ajali na athari za ufanywaji wa hiyo kazi ya Bodaboda inavyowafanya waamke saa kumi usiku na kurudi nyumbani saa tano usiku.

Lema alikuwa sahihi sana kwa kuongea ukweli, ila Siasa ni mchezo mchafu.

Wahitimu wa vyuo wanakosa ajira na kuishia kuwa Bodaboda, kazi ambayo ukizeeka hupati Mafao ya Pensheni, lakini watu wanajionea sawa tu.
 
Back
Top Bottom