Unaposema boda boda ni kazi ya laana, kusajili laini ni kazi ya kipuuzi hutaki mwanao umuone anaifanya utamfukuza kwako, vikoba ni laana sijui hutaki mkeo ajihusishe navyo kabisa.
From a standing point wewe ni mkimbizi wa kisiasa umebebwa huko Canada for over a year. Umepata PR na familia yako na privileges nyingi huko. Umeyaona maisha kwa utofauti hilo hatukatai. Najua kwa sasa wewe watoto wako wanaweza wakaishi huko Canada for whatever reasons, huko ada hazilipwi ni serikali kila kitu. Mzazi kazi yako ni kulipa kodi ya nyumba na utilities tu.
Viwanda na Private companies ziko kibao kiasi kwamba ishu ya kupata cha kufanya wakimaliza vyuo ni wao kuamua tu kukaa kwenye corporate sphere, kwenda kuuza migahawa, kukwangua mabarafu na kutawaza wazee.Maybe sio kazi za hovyo atleast kwa uchumi wa Canada maana hata wazungu wenyewe wa huko hawazitaki.
That being said, wewe unapata wapi guts za kusema kuwa Watanzania wanafanya kazi za laana esp. Boda boda, wasajili line na wauza mboga wanaocheza vikoba? Okay, hizo kazi ni za laana atleast kwa fikra zako lakini ushajiuliza kuna ugumu kiasi gani kwa hapa Tanzania when it comes to making ends meet?
Sidhani kama una idea kwamba graduate aliyemaliza chuo anaetoka familia hohehae anapitia ugumu kiasi gani na fedhea ilioje pale anapokosa ajira na hana mtaji! Usicheze na maisha ya watu kabisa, huna ajira una mke na mtoto huna chanzo cha pesa unafikiria kitakachofuata nini?
Utakaa chini unaangalia familia iangamie? Boda boda ndio quick fix ya maisha yetu ya dhiki walau familia zile na maisha yaende, vikoba ndio quick fix ya mikopo ya benki bila masharti magumu.
Toa solution watu wafanye nini baada ya kuachana na hizo kazi za laana. Sio unaropoka hovyo tu bila kuwa na substance. Tanzania sio Canada watu wanakolipwa dollar 15-20 kwa kazi ya saa 1. Huku unapigishwa mzigo masaa 12 unalipwa elfu 4 na hamna kitu utaongea.