Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Asagwile Mwasongwe, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mjadala unaoendelea wa ushirikiano wa kimuziki kati ya wasanii wa dini na wale wa muziki wa kidunia (secular).
Katika video aliyorekodi na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii, Asagwile ametoa wito rasmi akiwaalika wasanii wote wa secular wanaotaka kufanya naye kazi ya pamoja (kolabo) kujitokeza, akisisitiza kuwa yuko tayari kushirikiana nao bila ubaguzi wala unafiki ili kutengeneza kazi zitakazomtukuza Mungu na kutoa hamasa kwa jamii.
Akifafanua msingi wa msimamo wake, Mwasongwe ameeleza kuwa lengo kuu la mwimbaji wa Injili halipaswi kuwa kuwatenga au kuwahukumu wasanii wa secular kama "giza", bali ni kuwafikia kwa upendo na neema ya Mungu.
Akirejea kifungu cha Bibilia kutoka Yohana 1:5 kinachosema nuru uang'aa gizani na giza halikuweza, ameeleza kuwa mwimbaji wa Injili akiwa kama nuru ana wajibu wa kumvuta aliye gizani badala ya kuogopa kushirikiana naye.
Aidha, akionyesha fedha taslimu mkononi mwake, alibainisha kuwa fedha hutumiwa na kila mtu bila kujali imani, lakini zikipatikana na kupelekwa madhabahuni hutakaswa kwa neno la Mungu na maombi, huku akihitimisha kuwa shabaha yake kuu katika kolabo hizo ni kuhakikisha msanii anayeshirikiana naye anaongozwa kwenye sala ya toba na kupokea wokovu.