Bundakwetu
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 551
- 1,014
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala.
Hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa.
Na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela.
Kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela, kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu. Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.